Wauzaji dawa vyombo vya usafiri waonywa

WAUZAJI wa dawa za binadamu, vifaa tiba na mifugo wanaouza kupitia vyombo vya usafiri wameagizwa kuacha kuuza bidhaa hizo mara moja ili kuzuia madhara kwa binadamu pale wanapozitumia kutokana na kutokithi vigezo

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Katibu Tawala Msaidizi anayehusika na Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Frank Mmbando katika ufunguzi wa kikao kazi cha wadau ambao ni waingizaji wa dawa, vifaa tiba kuhusu kukidhi takwa la sheria ya dawa na vifaa tiba sura namba 219 yanayotolewa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kaskazini.

Mmbando amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wachuuzi wa dawa za binadamu kutumia vyombo vya usafiri kutangaza kuwa dawa fulani inatibu mgongo, kichwa na nk na wananchi wakinunua pasipokujua baada ya kuitumia ina madhara gani kiafya.

“Natoa onyo kwa wafanyibiashara wanaochuuza bidhaa hizo si kwa wale wanaobeba vikapu na kuingia navyo kwenye basi hata wale wanaowatuma kuuza wote watachukuliwa hatua”

Naye Meneja wa TMDA Kanda ya Kaskazini, Proches Patrick amesema mamlaka hiyo inadhibiti ubora na ufanisi wa dawa za binadamu, mifugo vifaa tiba na vitendanishi kwalengo la kuhakikisha vinaleta ufanisi zaidi

Amesisitiza kuwa TMDA inatoa elimu kwa wadau wanaotengeneza , wanaouza na kuingia bidhaa hizo katika maeneo mbalimbali ili waweze kuzingatia matakwa ya sheria ya dawa na vifaa tiba sura namba 219 kwa kuhakikisha bidhaa hizo zinakidhi vigezo katika kumfikia mwananchi ambaye anatumia dawa hizo kwa ugonjwa unaomsumbua kwa kupata dawa sahihi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button