PURA, ALNAFT wakutana Algiers kujadili namna ya kuinua sekta ya gesi asilia

Wawakilishi wa mamlaka hizo wamekutana jijini Algiers kujadili namna ya kushirikiana na kubadilishana uzoefu

Algiers, Algeria: Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA) imekutana na kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli ya Nchini Algeria (ALNAFT) kwa lengo la kqujadili namna ya kuanzisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika eneo la udhibiti wa shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

Mkutano huo uliofanyika jijini Algiers, Jumapili (Septemba 7, 2025), ulihudhuriwa na Rais wa ALNAFT, Samir Bekhti, huku Shigela Malosha  akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mhandisi Charles Sangweni, akiongoza ujumbe wa viongozi na wataalam kutoka Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho, Malosha alieleza kuwa ushirikiano baina ya taasisi hizo ni muhimu kwa ustawi wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli nchini Tanzania na Algeria kwa kuwa yatawezesha taasisi hizo kuongeza ufanisi wa shughuli za udhibiti na usimamizi wa masuala ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

“Kupitia kujengeana uwezo kwa njia ya mafunzo na kubadilishana uzoefu wa namna PURA na ALNAFT zinatekeleza majukumu, ni dhahiri kuwa mashirikiano haya yatakuwa chachu ya taasisi hizi kufanya vizuri zaidi” alisema Shigela.

SOMA:Mkurugenzi Puma ashauri wakuu taasisi za umma kuepuka urasimu 

Kwa upande wake, Rais wa ALNAFT alibainisha kuwa mashirikiano ya taasisi hizi ni muhimu na yatakuwa na manufaa makubwa kwa pande zote kwa kuzingangia kwamba PURA na ALNAFT zinatekeleza majukumu yanayofanana ingawa katika nchini tofauti.

Miongoni mwa maeneo ambayo PURA na ALNAFT zimejadili kubalishana uzoefu na kujengeana uwezo ni pamoja na udhibiti na usimamizi wa shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia, uhifadhi wa data za petroli, ushiriki wa kampuni za ndani katika miradi ya mafuta na gesi asilia na uandaaji wa sheria, kanuni na miongozo husika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button