Wazanzibari wahimizwa kuchagua amani

MGOMBEA ubunge Jimbo la Kiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hemed Suleiman Abdulla ametoa mwito kwa Wazanzibari, wachague amani badala ya vurugu.

Abdulla alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni za mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Mwinyi uliofanyika katika Viwanja vya Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba juzi. Alisema baadhi ya viongozi wamekuwa wakihubiri fujo na uvunjifu wa amani, ambayo itakwenda kuwaathiri wananchi wa Zanzibar.

Wananchi wa Zanzibar na hasa wale wa vyama vingine watafakari, waangalie, ndipo waamue kuchagua maendeleo badala ya kuchagua vurugu. Nayasema haya kwa sababu Pemba yamefanyika mambo ambayo hayakuwa na tija na badala yake ni athari kwa wananchi,” alisema Abdulla.

Alisema endapo mtu atavunja sheria, atachukuliwa hatua lakini akidumisha amani na upendo kutakuwa na upendo wa Mungu. “Niwaombe wananchi mkayasikilize yale yanayozungumzwa na wagombea lakini yale yanayozungumzia uvunjifu wa amani, basi msiyafuatishe. SOMA: ZEC yawateua wagombea 11 Urais Zanzibar

Nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na taratibu zake. Pia, mkasikilize kwa umakini sera za Mgombea wa urais Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi,” alisema Abdulla. Alisema CCM imekusudia kuendelea kunadi sera zake kwa kueleza waliyoyafanya na wanayotarajia kuyafanya, wakipata ridhaa ya kushika madaraka.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button