Wazee Tanga waasa vijana

Wazee jijini Tanga wamewashauri vijana kuacha mihemko katika maamuzi badala yake wasikilize ushauri wa watu waliowazidi umri ambao wana ukomavu na busara.

Wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari Mwenyekiti wa wazee Jiji la Tanga, Salum Bawazir amesema athari za maamuzi mabaya yaliyotokana na ushawishi ndio yamesababisha vurugu Octoba 29.

Hivyo amewataka vijana kuwa makini na watu wenye nia ovu ya kuwatumia vibaya na hivyo kusababisha changamoto ya uvunjifu wa amani.

“Madhara yaliyotokea nyote ni mashahidi hivyo sisi wazee wa Tanga tunawataka vijana kuacha kujihusisha kwenye vitendo vyote vya uvunjifu wa amani bali wahakikishe wanakuwa walinzi wa amani yetu, “amesema Bawazir.

Nae Samwel Kamote amesema amani ndio msingi wa taifa hivyo itakapoharibiwa kutatokea madhara makubwa ikiwemo kuyumba kiuchumi na maendeleo.

Nae Aziza Ramadhani amewataka vijana kuitumia Wizara ya Vijana kama sehemu ya daraja lao la kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili ili serikali iweze kuwasaidia

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Tanzania: Rais wa Ujerumani akabiliwa na historia ya ukoloni wa nchi yake.

    Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier siku ya Jumanne ametetea “kazi ya pamoja” na Tanzania kuhusu “ukurasa mbaya” wa ukoloni wa nchi hii ya Afrika Mashariki na Ujerumani, na kufungua njia ya kurejesha mali iliyoporwa.

  2. Rais Frank-Walter Steinmeier siku ya Jumatano alielezea “aibu” yake kwa uhalifu uliofanywa wakati wa utawala wa kikoloni wa Ujerumani nchini Tanzania na kuahidi kuongeza ufahamu kuhusu uhallifu uliotendwa na nchi yake.

    Rais wa Ujerumani aomba msamaha kwa Watanzania kwa yaliyofanywa na utawala wa kikoloni
    Rais wa Ujerumani aomba msamaha kwa Watanzania kwa yaliyofanywa na utawala wa kikoloni ‘Napenda kuomba msamaha kwa kile ambacho Wajerumani waliwafanyia mababu zenu hapa,” alisema Steinmeier alipotembelea Makumbusho ya Maji Maji, katika mji wa kusini wa Songea, kulingana na nakala ya hotuba yake

    Tanzania ilikuwa sehemu ya German East Africa ambayo ilishuhudia uasi wa umwagaji damu zaidi katika historia ya ukoloni kati ya 1905 na 1907.

    Wataalamu wanasema kati ya watu 200,000 na 300,000 wazawa wa eneo hilo waliuawa kikatili wakati wa kile kinachoitwa Uasi wa Maji Maji, hususani kutokana na uharibifu wa mashamba na vijiji uliofanywa na wanajeshi wa Kijerumani.

  3. Rais wa Ujerumani aomba msamaha kwa Watanzania kwa yaliyofanywa na utawala wa kikoloni

    Rais Frank-Walter Steinmeier siku ya Jumatano alielezea “aibu” yake kwa uhalifu uliofanywa wakati wa utawala wa kikoloni wa Ujerumani nchini Tanzania na kuahidi kuongeza ufahamu kuhusu uhallifu uliotendwa na nchi yake.

    “Napenda kuomba msamaha kwa kile ambacho Wajerumani waliwafanyia mababu zenu hapa,” alisema Steinmeier alipotembelea Makumbusho ya Maji Maji, katika mji wa kusini wa Songea, kulingana na nakala ya hotuba yake

    Tanzania ilikuwa sehemu ya German East Africa ambayo ilishuhudia uasi wa umwagaji damu zaidi katika historia ya ukoloni kati ya 1905 na 1907.

    Wataalamu wanasema kati ya watu 200,000 na 300,000 wazawa wa eneo hilo waliuawa kikatili wakati wa kile kinachoitwa Uasi wa Maji Maji, hususani kutokana na uharibifu wa mashamba na vijiji uliofanywa na wanajeshi wa Kijerumani.

    “Kilichotokea hapa ni historia yetu ya pamoja — historia ya mababu zenu na historia ya mababu zetu huko Ujerumani,” alisema, akiahidi “kuzichukua hadithi hizi pamoja nami hadi Ujerumani, ili watu wengi zaidi katika nchi yangu wazijue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button