Waziri Mkenda aikabidhi TISTA vitabu elimu ya dini

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amekabidhi vitabu vya elimu ya dini ya kiislamu kwa ngazi ya elimu ya sekondari kwa Taasisi ya Kusimamia Ufundishaji wa Elimu ya Dini ya Kiislamu (TISTA).

Makabidhiano hayo yalifanyika Januari 11, 2026, katika Ofisi za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es Salaam, ambapo Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi, akiongozana na viongozi wengine, amepokea vitabu hivyo kwa niaba ya TISTA.

Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkenda amesema Serikali imekabidhi jumla ya nakala 5,000 za vitabu vya kiada vya Somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa Kidato cha Pili vyenye thamani ya Sh milioni 16 pamoja na nakala 1,000 za vitabu vya mwongozo wa mwalimu vyenye thamani ya Sh milioni 1.2.

Ameeleza kuwa serikali itaendelea kuchapisha na kusambaza vitabu vya kidato cha sita pamoja na vile vya kidato cha tatu na cha nne pindi vitakapokamilika, na kuipatia BAKWATA nakala kwa ajili ya kusambazwa katika shule zisizo za Serikali Tanzania Bara na Zanzibar.

Prof. Mkenda ameishukuru TET kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na TISTA na kuhakikisha inagharamia kikamilifu uandishi na uidhinishaji wa vitabu vya elimu ya dini ya kiislamu.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya dini nchini ili kuhakikisha elimu ya dini inafundishwa kwa ufanisi na kuchangia kujenga Mtanzania mwenye maadili mema.\

Kwa upande wake, Sheikh Abubakar Zuberi, ameishukuru serikali kwa ushirikiano uliowezesha kukamilika uandaaji wa maudhui ya vitabu vya slimu ya dini ya kiislam

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Hi! I know this is somewhat off topic but I was wondering if you knew where I could locate a captcha plugin for my comment form?
    I’m using the same blog platform as yours and I’m having problems finding one?
    Thanks a lot!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button