Wenye afya ya akili wapelekwe vituo vya afya

DAR ES SALAAM : JAMII imeshauriwa kuchukua hatua za haraka kwa kuwafikisha kwenye vituo vya afya watu wenye afya ya akili pamoja na kuwapa elimu.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani, mwakilishi wa Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es salaam, Dk.Gunini Kamba amesema jamii inapaswa kutambua kuwa jukumu la changamoto ya afya ya akili linapaswa kuchukuliwa na kila mmoja.

Ameongeza kuwa katika kuondokana na changamoto hiyo ni vyema pia jamii kujenga utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara angalau mara tatu kwa wiki.
Kiongozi wa Mradi wa Choice unaoshughulikia changamoto za afya na masuala yanayohusiana na afya unaoratibiwa na Hospitali ya Aghakhan, Profesa Ahmed Jusaban amesema upo umuhimu wa jamii kutambua changamoto ya afya ya akili hususani mahala pa kazi ili kuongeza umakini katika utendaji kazi.

Wadau walioshiriki maadhimisho hayo ni Mkurugenzi wa Marcus Mwemezi Foundation, Belinda Nyapili na Mkurugenzi wa Lisa Jensen Foundation LISA ZAGAR wanaoshughulikia changamoto ya afya ya akili.




