WAKALA wa Uhifadhi wa Misitu (TFS) wameahidi kudhibiti vikwazo kwa watumishi wenye vipaji badala yake watawapa nafasi ili kuwa wanamichezo bora ndani na nje ya nchi ikiwemo michezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)
Hayo yamesemwa na mratibu wa dawati la bonanza hilo kutoka TFS ambaye ni Ofisa Mhifadhi Mwandamizi , Marcel Bitulo ameeleza kuwa bonanza hilo ni muhimu maeneo ya kazi kwani michezo ni kichocheo kikubwa cha kuimarisha mwili.
Amesema mchezaji yoyote atakayeonekana kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ataendelezwa ili kutimiza ndoto zake sanjari na kukata fursa ya kushiriki mashindano ya ndani na nje ya nchi ikiwemo nchi za EAC
“Michezo ni ajira na bonanza hili tulilolindaa ni mahsusi kwa aajili ya kuibua vipaji kwa watumishi katika riadha,mpira wa miguu na mashindano mengine ikiwemo mpira wa mikono ambapo jumla ya washiriki zaidi ya 250 kutoka katika kanda nane za uhifadhi nchini wanaonyesha vipaji vyao kwaaajili ya kujiweka mguu sawa na shimuta
Naye mshiriki wa mbio za mita 100, Grace Kimario ambaye ni Ofisa Misitu Msaidizi kutoka wilayani Songea amesema ameshinda riadha na kuwa mshindi wa kwanza na kutoa rai kwa taasisi nyingine kufanya bonanza hilo la michezo ili kuimarisha mwili na kuondoka msongo wa mawazo mpira wa miguu,mikono pamoja na riadha.
“Nipende kuelekeza katika kila kanda kutenga bajeti ambazo zitaweza kuwezesha shughuli za michezo kwa askari wetu wa uhifadhi ikiwa ni njia pekee ya kuendelea kuimarisha afya kwa askari wetu”
Huku Michael Karai ambaye ni mshindi wa kilomita 5 kutoka TFS Songea kituo cha Madaba alishukuru kushiriki mashindano hayo, aliomba TFS kuweka kambi ya zaidi ya siku nne au tatu ili kuwawezesha wachezaji kuonesha vipaji vyao.