Wenyeviti waagizwa kuwa karibu na wananchi

WENYEVITI wa vijiji na vitongoji wilayani Monduli wametakiwa kuwa karibu na wananchi na kuhakikisha wanasikiliza na kutatua changamoto zao ili kuondoa malalamiko na kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na serikali.

Agizo hilo limetolewa katika kijiji cha Mti Mmoja, kata ya Sepeko wilayani Monduli na Mkuu wa Wilaya hiyo, Gloriana Kimath, wakati wa mkutano wa kusikiliza na kujibu kero za wananchi uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya mtendaji wa kijiji hicho.

Akizungumza katika mkutano huo, Kimath amesema iwapo viongozi wa ngazi hizo watakuwa mstari wa mbele kushughulikia kero za wananchi, kutasaidia kuondoa malalamiko, kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Amesema kiongozi ambaye hawezi kukaa karibu na wananchi anapaswa kupisha nafasi hiyo ili kupatikane mtu mwenye dhamira na uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa ukaribu na ufanisi. SOMA : Waliompiga askari kusakwa Monduli

Aidha, amebainisha kuwa lengo la ziara yake kijijini hapo ni kujitambulisha kwa wananchi pamoja na kusikiliza, kutatua na kufuatilia changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki kutoka kwa serikali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button