Yanga, Coastal, Ihefu zatinga Nusu Fainali

DAR ES SALAAM;TIMU za Yanga, Coastal Union na Ihefu zimetinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya leo kushinda michezo yao ya Robo fainali.

Ihefu imefuzu hatua hiyo baada ya kuitoa Mashujaa ya Kigoma kwa penalti 4-3 baada ya timu hizo kutoka 0-0 katika dakika 90 mchezo uliofanyika Uwanja wa Liti, Singida, huku Coastal ikifuzu baada ya kuifunga Geita Gold bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Yanga yenyewe imefuzu Nusu Fainali baada ya muda mfupi uliopita kuifunga Tabora United mabao 3-0 Uwanja wa Azam Chamazi, ambapo timu ya nne itajulikana Ijumaa Mei 3, wakati Azam itakapocheza na Namungo katika uwanja huohuo.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Azi Ki dakika ya 35, Kennedy Musonda dakika ya 66 na Joseph Guede dakika ya 83.

Habari Zifananazo

Back to top button