Zahanati kupunguza vifo vya wajawazito

KIGOMA: KUKAMILIKA kwa Zahanati ya Lemba iliyopo Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kutapunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kutokana na hapo awali kufuata huduma za afya umbali mrefu.

Mkuu wa Wilaya Buhigwe, Michael Ngayarina amesema hayo akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Ismail Alli Ussi wakati ukianza mbio zake wilayani Buhigwe kutembelea miradi mbalimbali.

Ngayarina amesema kuwa kabla kujengwa kwa zahanati hiyo wananchi walikuwa wakitembea kilometa nane kuelekea kijiji cha Muyama katika wilaya hiyo ya Buhigwe kufuata huduma hiyo ya matibabu au kutembea kilometa 18 kwenda kupata huduma katika Kituo cha Afya Shunga Wilaya ya Kasulu jambo ambalo lilikuwa usumbufu mkubwa.

Kutokana na changamoto hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa wananchi walianza kuchangishana wenyewe ili kuanza kutekeleza mradi huo ndiyo serikali kuu, Halmashauri na wadau mbalimbali wakawaunga mkono na kukamilisha mradi huo hadi kuanza kutoa huduma ambapo milioni 130 zimetumika hadi kukamilika.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Uhuru, Ismail Alli Ussi aliwapongeza wananchi wa kijiji hicho na kusema kuwa moyo wa kizalendo ndiyo uliowasukuma kufanya hivyo na kuwataka kuendelea kujitolea kwa hali na mali katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.

Ussi amesema kuwa pamoja na jitihada hizo serikali imeendelea kutekeleza kwa kuanzisha miradi mipya ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi lakini pia kumalizia miradi ikiwemo ya utoaji huduma iliyoanzishwa na wananchi ukiwemo mradi huo wa Zahanti ya Lemba wilayani Buhigwe.

Habari Zifananazo

6 Comments

  1. YALIYOJIFICHA MOCHWARI, HATOSAHAU, MAITI KUFUFUKA, KUPAKWA MAKEUP ALIEKAA MIAKA 7 ANAHUDUMIA MAITI
    542,245 views · 4 years ago…more

  2. YALIYOJIFICHA MOCHWARI, HATOSAHAU, MAITI KUFUFUKA, KUPAKWA MAKEUP ALIEKAA MIAKA 7 ANAHUDUMIA MAITI
    542,245 views · 4 years ago…more

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button