Zaidi ya vijiji 10,000 vinapata maji safi – Aweso

TANGA: WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema Rais Samia ameweza kumtua mama ndoo kichwani kwani kati ya vijiji 12,318 vilivyopo nchini tayari vijiji 10,818 vinapata huduma ya maji safi na salama.

Aweso amesema hayo leo Juni 14 Mwenge wa Uhuru ulipofika katika kijiji cha Mikocheni kuweka Jiwe la Msingi katika mradi wa maji Mikocheni kuelekea Mkwaja wilayani Pangani.

Amesema kuwa vijiji vilivyobaki 1,500 vipo kwenye mpango wa kupelekwa huduma ya maji kupitia utekelezaji wa miradi ambayo inaendelea kutelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini.

“Wizara ya Maji tumepanga kumheshimisha Rais Samia kupitia sekta hiyo kuhakikisha mpaka mwishoni mwa mwaka huu vijiji vyote nchini vinakuwa na huduma safi na salama,”amesema Waziri Aweso.

Hata hivyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali ussi amewapongeza Wakala wa Huduma ya Majisafi Mijini na Vijijini (RUWASA) kwa kusimamia vizuri miradi ya maji.

“Niwapongeze RUWASA mmekuwa wazalendo sana katika utekelezaji wa miradi ya maji kwani kwenye mikoa 10 ambayo mwenge wa uhuru imepita sekta ya maji mmekuwa na miradi yenye ubora sana”amesema kiongozi huyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button