Zaidi ya watu 5,000 kuhudhuri maonesho ya kuku Dar

ZAIDI ya watu 5000 kutoka ndani na je ya nchini wanatarajiwa kuhudhuri maonesho ya kuku na ndege wafungwa yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 10 hadi 11,2025 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kuhusu maonesho hayo, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Uzalishaji Vyakula vya Mifugo Tanzania(TAFMA) na Mjumbe wa Kamati inayoandaa Maonesho ya Kuku na Ndege Wafungwa, Sufian Kyarua amesema maonesho hayo yataambatana na mafunzo kwa wafugaji ili kufanya ufugaji wa kisasa.
“Lengo ni kuhakikisha wafugaji wetu wanaongeza ujuzi na utaalamu ili kuhakikisha wanafunga kwa faida na kuhakikisha mazao yao yanakuwa ni salama kwa walaji.
Ameongeza “Haya ni maonesho ya tisa tulianza 2015 tumekuwa tukipata mafanikio kila mwaka hii inaonesha wafugaji wetu pamoja na walaji wanahamu ya kujua bidhaa tunazozalisha.
Amesema katika maonesho ya mwaka huu washiriki ni wengi ambapo mpaka sasa wana washiriki 62 kutoka nje ya nchi zaidi ya 10 Duniani na washiriki wengi wa ndani.
Kyarua amebainisha kuwa wana washiriki waliojiandikisha kutoka nchi za Ujerumani, Hungary, Uholazi, Ufaransa, Ubelgiji, India ,China,Kenya na Morocco.
Ameeleza kuwa changamoto zilizopo ni upatikanaji wa elimu sahihi kuhusu namna bora ya ufugaji na kupata faida.
“Nyingine ni kwa walaji hawaamini kuku wa nyama wakifungwa kwa muda wa wiki nne na kufikia uzito wa soko wanahisi kuna dawa zinatumika jambo ambalo sio kweli,”amesisitiza.
Amesema ufugaji wao umejikita katika aina tatu ambapo sehemu ya kwanza ni jenetiki kwamba kuku wanaofuga ni wale ambao wamechaguliwa kitaalamu wanauwezo wa kula chakula chache wakatoa mayai mengi au kutengeneza nyama nyingi.
“Aina ya pili ni wale kuku ambao wanapewa lishe na vyakula tunavyotengeneza yanakidhi mahitaji yao tunazingatia virutubisho vyote na tatu ni mazingira wanayofungwa maji safi na salama,hewa ya kutosha,chanjo ili kuhakikisha badala ya kuwatibu tunazuia magonjwa.
Amesema kwa maonesho yaliyopita kulikuwa na watu 4000 na kila mwaka mwitikio ni mkubwa wafugaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi watakuja kuangalia teknolojia.
Kyarua amefafanua kuwa elimu wanayotoa ni ya ndege wote wanaofungwa kama kuku,bata,Kanga,njiwa akisisitiza kuwa uhitaji wa soko unaongezeka hivyo ni muhimu kuongeza uzalishaji.
“Kwa watani wa shirika la Afya Duniani (WHO) mtu mmoja anatakiwa kula mayai 300 lakini mpaka sasa katika nchi yetu ni 106 kwenye nyama mtu anatakiwa kula angala kilo 50 lakini sasa kwa nyama za kuku kilo tatu bado hizijafika kwa mtu mmoja.



