Zitto aahidi mikopo bila riba kwa wajasiriamali

KIGOMA: MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameahidi kuanzisha mfuko maalumu wa mikopo bila riba kwa wajasiriamali.

Zitto Kabwe amesema hatua hiyo itakomesha mikopo yenye riba kubwa maarufu ‘kausha damu’ endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Akizungumza leo Septemba 18 , 2025 katika kampeni zake Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji, Zitto amesema katika kufanikisha hilo atatoa Sh bilioni 1 ili wananchi wakope.

Viongozi, wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo na wananchi wa Manispaa ya Kigoma wakifuatilia kampeni za mgombea Zitto Kabwe uliofanyika eneo la Kagera Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mgombea huyo amesema kuwa mikopo yenye riba kubwa imekuwa changamoto kubwa kwa wajasiliamali kwani huwafanya shughuli zao kukua kwa tija lakini pia taratibu zao hazina utu na staha na wakati mwingine kunyang’anywa mali zao kwa kushindwa kurudisha mikopo kwa wakati.

Amesema kuwa mpango wa utoaji mikopo ni sehemu ya mambo ya kipaumbele atakayoshughulikia ikiwa ni pamoja na kuanzisha mpango wa hifadhi ya jamii ambao ndani yake kutakuwa na taratibu za utoaji mikopo kwa wajasiliamali na huduma za afya kwa ajili ya matiababu kwa wote.

Mgombea udiwani wa Kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji, Kana Abdallah (kushoto) akizungumza mkutano wa hadhara wa kampeni ya mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (kulia) uliofanyika eneo la Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji

Aidha, katika ahadi zake mgombea ubunge huyo wa Jimbo la Kigoma Mjini amesema kuwa wakipewa ridhaa ya kushika Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji kwa kuwa na mbunge na idadi kubwa ya madiwani wataligeuza eneo la Kagera Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji kuwa Satelite City (Mji wa pembeni wenye huduma muhimu za kijamii) hivyo ameomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua ili kuweza kutekeleza mipango hiyo.

Kwa upande wake Mgombea udiwani kata ya Kagera Manispaa ya Kigoma Ujiji, Kana Abdallah alisema akichaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo jambo la kwanza itakuwa kupigania malipo ya fidia ya wananchi ambao maeneo yao yalichukuliwa na Mpango wa Uwekezaji (KISEZ) lakini malipo imekuwa na vurugu.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am making a real GOOD MONEY ($100 to $120 / hr) online from my laptop. Last month I GOT cheek of nearly 19840$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. You become independent after joining this JOB. I really thanks to my FRIEND who refer me this SITE….., http://Www.Cashprofit7.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button