ZMBF Yapongeza Sanaa na Ubunifu Sharjah

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam H. Mwinyi, ametembelea House of Wisdom mjini Sharjah, maktaba ya kisasa inayohifadhi zaidi ya vitabu 300,000 vya kielimu, fasihi na tafiti mbalimbali.

Katika ziara hiyo, amejionea namna mashairi ya kale yanavyowasilishwa kwa kutumia teknolojia na ubunifu wa kisasa unaovutia vijana kujifunza na kutumia historia katika maendeleo. Aidha, Mama Mariam ametembelea Soko Asili la Al-Asra ambako alishuhudia kazi za mikono zinazotengenezwa na wasanii wa ndani, wakiwemo vijana wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo.

Katika ziara hiyo alivutiwa na ubunifu wao katika utengenezaji wa misala, pochi, vikombe vya kahawa na bidhaa nyingine zinazobeba utamaduni wa Kiemarati. Ziara hiyo imeonesha dhamira ya Mama Mariam Mwinyi katika kuunga mkono sanaa, fasihi, utamaduni na ubunifu kama nyenzo za maendeleo na uwezeshaji wa jamii, hususan makundi maalum. SOMA: Zanzibar Yatajwa Kuwa Daraja la Utamaduni

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button