16 wapandikizwa nyonga, magoti bandia

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar, wameendesha kambi maalum ya upasuaji wa kupandikiza goti na nyonga bandia ambapo zaidi ya wagonjwa 16 wamefanyiwa upasuaji katika kpindi cha siku tano.

Kambi hiyo imefanyika ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano kati ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja na MOI wenye lengo la kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi.

Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Mazrui amesema kambi hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Hussein Ally Mwinyi la kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa na kibobezi, bila kulazimika kuzifuata huduma hizo Dar es Salaam au nje ya nchi.

“Leo ni siku ya pekee kwani tumekutana hapa kueleza matunda ya ushirikiano kati ya Hospitali yetu ya Mnazi Mmoja na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili-MOI, kama mnavyofahamu mwezi Novemba mwaka jana ushirikiano huu ulianza na leo tunashuhudia matunda yake, ambapo madaktari bingwa na wauguzi kutoka MOI wamekuja hapa Zanzibar kuwahudumia wananchi wetu,” amesema  Mazrui.

Kwawa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dk Muhiddin Mahmoud amemshukuru Rais wa  Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Hussein Mwinyi pamoja na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Mazrui kwa usimamizi imara kwenye sekta ya afya.

Pia Dk Muhiddin amemshukuru Mkurugenzi Mtandaji wa MOI Prof. Abel Makubi kwa kuridhia kuanzisha ushirikiano na hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar pamoja na kutuma jopo la madaktari bingwa wabobezi pamoja na wauguzi wabobezi kutoa huduma kwa wananchi wa Tanzania visiwani.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dk. Violet Lupondo, amesema MOI imekua ikitekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kuhakikisha huduma za kibingwa za MOI zinasogezwa karibu na wananchi, ambapo kwa sasa huduma hizo zinapatikana katika maeneo mbalimbali hapa nchini, ili kuwapunguzi awananchi usumbufu wa kufuata huduma MOI Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button