Wanne familia moja wafariki kwa moshi wa jenereta

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la vifo vya watu wanne wa familia moja ambao wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa chafu ya moshi kutoka kwenye jenereta.

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro Jumanne  leo  April 20, 2023 jijini Dar es Salaam amesema tukio hilo lilitokea siku ya jana maeneo ya Temeke ambapo familia hiyo iliwasha jenerata ndani ya nyumba na baadae kulala.

“Majira ya saa 4 :00 usiku watu hao waliwasha jenereta baada ya umeme kuzimika na kuliweka ndani ya nyumba.

Advertisement

”Amesema

Muliro amesema, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu hao walipoteza maisha baada ya kuvuta hewa inayodaiwa kuwa ni hewa chafu ya moshi iliyokuwa inatoka kwenye jenereta baada ya kuwashwa.

Aidha, aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Kazija Mohamed (21), Munir Ibrahim (7), Munira Ibrahim (6) Muyyat Ibrahim (3).

Pia alisema Mume na Mke waliofahamika kwa majina ya Ibrahim Juma (28) na Aisha Ayubu (29) hali zao sio nzuri na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *