22 mbaroni wakidaiwa kuvamia mgodi tanzanite

MENEJA wa Mgodi wa Gem & Rock Venture, Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti ametiwa mbaroni na wenzake 21 kwa tuhuma za kuongoza genge la wachimbaji wadogo ‘Wana Apollo’ na kuvamia mgodi wa madini ya tanzanite uliopo Kitalu C katika Mji wa Mirerani, wilayani Simanjiro.

Mgodi wa Kitalu C unaochimbwa kwa ubia kati ya serikali na mwekezaji mzawa, Onesmo Mbise ulivamiwa Machi 12 mwaka huu na kuwajeruhi zaidi ya wafanyakazi 10 wa kampuni ya Franone.

Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara, George Katabazi alisema kuwa polisi imefanikiwa kumkamata Saitoti, ambaye inadaiwa kuwa ndio kiongozi mkuu wa uvamizi huo na bado anahojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Mirerani.

Alisema mbali ya Saitoti kuna wana Apollo wengine wamekamatwa, ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Gem & Rock Venture, kampuni inayomiki mgodi wa tanzanite ulipo kitalu B mpakani mwa mgodi wa Kitalu C.

Alisema kama taratibu za upelelezi na mahojiano zikikamilika huenda wakafikishwa mahakamani mapema kujibu mashitaka.

‘’Tumemkamata Saitoti ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Gem & Rock Venture na pia ndio aliyekuwa kiongozi wa kuongoza genge la wavamizi katika mgodi wa serikali na mbia mwenza’,’alisema Katabazi.

Habari Zifananazo

Back to top button