Tanzania kushiriki mkutano mabadiliko tabianchi

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ameihakikishia Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa Tanzania itashiriki Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) mwezi Disemba 2023.

Makamba amesema hayo alipokutana na kuzungumza na Waziri wa Viwanda na Tekinolojia ya Juu wa UAE, Sultan Ahmed Al Jaber jijini Nairobi, Kenya.

Waziri Makamba amekutana na Al Jaber pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaofanyika nchini humo.

Advertisement

Amesema miongoni mwa masuala itakayoyatilia mkazo ni ufadhili wa miradi ya nishati safi ya kupikia kwa akina mama vijijini.

Waziri Makamba amesisitiza kuwa Tanzania itaungana na nchi za Afrika na nchi nyingine zinazoendelea duniani, kuhimiza nchi Wanachama, hususani zilizoendelea kutekeleza ahadi za kupunguza hewa ukaa, kuchangia fedha kwa ajili ya uhimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na upatikanaji wa teknolojia kwa ajili ya jitihada hizo.

7 comments

Comments are closed.