Mbumba Rais mpya Namibia
RAIS mpya wa Namibia, Nangolo Mbumba leo ameapishwa kuwa rais wa nne wa taifa hilo baada ya rais Hage Geingob kufariki leo Jumapili.
Kiongozi huyo aliyewahi kuhudumu kama makamu wa rais chini ya Serikali ya Rais Geingob amekula kiapo katika Ikulu ya nchi hiyo.
Mbumba alitoa pongezi kwa mtangulizi wake akimtaja kuwa mbunifu mkuu wa katiba na usanifu wa utawala wa Namibia.
pharmacy
Mbumba ameapishwa kuwa Rais wa Namibia na Jaji Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Namibia na atakuwa Rais hadi pale Uchaguzi Mkuu utakapofanyika baadaye mwaka huu.