Watu 17 wauawa kwa risasi Afrika Kusini

AFRIKA KUSINI: WATU 17 wameuawa kwa kupigwa risasi katika matukio mawili tofauti nchini Afrika Kusini, huku nchi hiyo ikiendelea kukabiliwa na kiwango kikubwa cha mauaji yanayohusishwa na uhalifu.
Kwa mujibu wa polisi, takwimu zinaonesha kuwa wastani wa watu 60 huuawa kila siku nchini humo, huku sababu za mauaji hayo zikihusishwa na biashara ya dawa za kulevya, uchimbaji madini usio rasmi pamoja na ushindani wa njia za usafirishaji wa abiria kwa kutumia mabasi madogo.
Katika tukio la kwanza, miili ya watu tisa ilikutwa Jumatatu asubuhi katika makazi yasiyo rasmi nje ya mji mkuu wa Pretoria. Msemaji wa polisi alisema wote walikutwa ndani ya kibanda wakiwa na majeraha ya risasi. Waliofariki ni wanaume sita na wanawake watatu.
Kwa mujibu wa mtandao wa Africanews, tukio la pili lilitokea katika eneo la pembezoni mwa mji wa Pietermaritzburg, mashariki mwa nchi hiyo, ambako polisi walikuta gari lililokuwa na mashimo ya risasi baada ya kupokea taarifa za ufyatulianaji risasi Jumapili usiku.
Taarifa ya polisi ilisema ndani ya gari hilo walikuta wanaume wanane wakiwa na majeraha mengi ya risasi na kuthibitishwa kufariki dunia eneo la tukio.
Msemaji wa polisi wa jimbo la KwaZulu-Natal, Kanali Robert Netshiunda, alisema wanaume hao walikuwa bado hawajatambuliwa na kwamba ilikuwa mapema kubaini sababu za mauaji hayo.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Newzroom Afrika, Netshiunda alisema matukio kama hayo yamewahi kutokea nchini humo, huku sababu zake zikitofautiana, ikiwemo wizi wa mifugo, biashara ya dawa za kulevya na migogoro inayohusisha usafirishaji wa abiria kwa mabasi madogo.




NEW88 – Nhà Cái Giải Trí Trực Tuyến Hàng Đầu, Mang Đến Trải Nghiệm Cá Cược Đẳng Cấp Với Kho Game Đa Dạng tại : https://new88-ok1.online
NEW88 – Nhà Cái Giải Trí Trực Tuyến Hàng Đầu, Mang Đến Trải Nghiệm Cá Cược Đẳng Cấp Với Kho Game Đa Dạng tại: https://jaya33.my