Dk. Mwinyi akutana na watendaji wa UNESCO

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Watendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO waliofika Ikulu Zanzibar leo, kwa mazungumzo kuhusu utekelezaji wa shughuli za elimu, sayansi, utamaduni na habari zinazoratibiwa na shirika hilo nchini.

Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Dk. Khamis Khalid Said, akiambatana na Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano na Habari, Bi. Christina Musarache. SOMA: Mwinyi aiomba UNESCO kusaidia uchumi wa Buluu Zanzibar

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walimwasilisha kwa Rais Dk. Mwinyi taarifa kuhusu shughuli za Tume ya Taifa ya UNESCO, ikiwemo maandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika Mkutano Mkuu wa UNESCO unaotarajiwa kufanyika nchini Uzbekistan kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 13, 2025.

Mazungumzo hayo yalilenga pia kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na UNESCO katika kuboresha sekta za elimu, utamaduni, sayansi na mawasiliano, sambamba na kukuza miradi ya maendeleo endelevu inayoendana na malengo ya kimataifa ya SDGs.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button