Zungu ndiye Spika wa Bunge

DODOMA : BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemchagua Mussa Azzan Zungu kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 378 kati ya kura 383 zilizopigwa leo mjini Dodoma.
Matokeo hayo yamethibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi mara baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika. Wagombea wengine walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho ni Chrisant Ndege wa Chama cha Democratic Party (DP), Veronica Charles wa NRA, na Amin Alfred wa ADC, ambao kila mmoja alipata kura sifuri.
Aidha, Anita Halfan Mgaya wa NLD na Ndonge Said Ndonge walipata kura moja kila mmoja, huku kura tatu zikiharibika. Kwa ushindi huo, Zungu anachukua rasmi nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kijacho cha uongozi. SOMA: Ndege Aahidi Bunge la Maendeleo



