Ndege Aahidi Bunge la Maendeleo

MGOMBEA wa nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Democratic Party (DP), Chrisant Ndege ameahidi kuligeuza Bunge hilo kuwa la maendeleo kwa kufanya kazi inayotokana na bajeti zitakazowasilishwa bungeni na Serikali ambayo malengo yake ni kuwaletea wananchi maendeleo. SOMA: Rais Samia Awateua Wabunge Sita

Ameyasema hayo bungeni Dodoma leo wakati akiomba kura kwa wabunge za kumchagua kuwa Spika. Pia ameahidi endapo atachaguliwa kuwa spika atalisimamia Bunge kuhakikisha miswada yote ya sheria inayowasilishwa bungeni kupitishwa kuwa sheria inazingatia maadili ya kitanzania na si vinginevyo.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button