Balozi Omar aeleza umuhimu sekta ya bima kiuchumi
WAZIRI wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar amesema sekta ya bima ina mchango mkubwa kukuza uchumi wa taifa hususani kulinda mali na shughuli za kiuchumi za wananchi na taasisi.
Balozi Omar alisema hayo Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ukiongozwa na Kamishna wa Bima Tanzania, Dk Baghayo Saqware.
Walijadili masuala ya maendeleo na mustakabali wa sekta ya bima nchini.
Alisema sekta hiyo ni nguzo muhimu katika ustahimilivu wa uchumi, ulinzi wa wananchi dhidi ya majanga na hatari mbalimbali pamoja na kuchochea uwekezaji na maendeleo endelevu.
Balozi Omar alibainisha kuwa sekta ya bima husaidia kuongeza imani ya wawekezaji, kulinda rasilimali za serikali na binafsi na kupunguza mzigo wa kifedha kwa wananchi wakati wa majanga.
“Muendelee kufanya kazi nzuri kwa jamii kama Sheria ya Bima Kifungu cha 5 (1) cha Sheria ya Bima, Sura ya 394 ilivyowapa majukumu ya kulinda haki za wadau wa bima, kutoa elimu kwa umma na kushughulikia malalamiko yao na kuendeleza soko la bima kwa kuhakikisha linakuwa salama, endelevu na stahimilivu,” alisema.
Kwa upande wake Kamishna wa Bima Tanzania, Dk Saqware, akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake alisema TIRA inaendelea kusimamia sekta ya bima kwa weledi na kuifanya sekta hiyo kuendelea kukua kwa wastani wa zaidi ya asilimia 10 kwa kipindi cha miaka minne.
Dk Saqware alisema mwaka 2024 ada za bima ziliongezeka na kufikia Sh trilioni 1.52 kutoka Sh trilioni 1.24 mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20.2 na mchango wa sekta ya bima kwenye Pato la Taifa kuongezeka kutoka asilimia 2.01 mwaka 2023 na kufikia asilimia 2.08 mwaka 2024.
Aidha, alieleza kuwa viashiria vya ukuaji wa sekta ikiwemo malipo ya madai, usajili wa watoa huduma na mali na uwekezaji, ajira na wanufaika wa bima vimeendelea kukua.
“Pamoja na mafanikio haya, TIRA tumeendelea kulipa gawio kwa serikali ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Shilingi bilioni 5.1 zilitolewa ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo gawio lilikuwa ni Shilingi bilioni 3.5 sawa na ongezeko la asilimia 68.6,” alisema.
Pande zote mbili zilijadili pia changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya bima pamoja na mikakati ya kuimarisha ushiriki wa wananchi na taasisi mbalimbali katika matumizi ya huduma za bima.
Aidha, walijadiliana masuala ya kisheria yanayoiongoza sekta hiyo, ikiwemo umuhimu wa kuendelea kufanya maboresho ya sheria na kanuni za bima ili ziendane na mabadiliko ya kiuchumi, teknolojia na mahitaji ya soko la sasa nchini.




I make up to $220 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $450h to $890h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now I am hoping I could help someone else out there by sharing this link.Try it, you won’t regret it!.
HERE→→→→→→→→→→ https://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com