Chelsea yamfuta kazi Maresca

ENGLAND: Klabu ya Chelsea imethibitisha kumfuta kazi kocha mkuu, Enzo Maresca, raia wa Italia.

Taarifa ya Chelsea imeeleza kuwa uamuzi huo unatoa taswira mpya ya kuirudisha timu kwenye ushindani na kushiriki mashindano makubwa ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Katika kipindi chake, Enzo aliiongoza klabu kwenye mafanikio ya mashindano ya UEFA Conference League na FIFA Club World Cup. Mafanikio hayo yatabaki kuwa kumbukumbu,” imeeleza taarifa hiyo.

Enzo alichukua jukumu la kuifundisha Chelsea Juni 2024 baada ya kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button