Prof. Jay atimiza miaka 50

MKE wa msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na mbunge wa zamani wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’, Grace Mgonjo maarufu kama ‘Mama Lisa’, amebainisha kuimarika kwa afya ya mume wake na kutoa matumaini ya kurejea kwake kazini ifikapo mwaka 2026.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kutimiza umri wa miaka 50 wa msanii huyo, Mama Lisa amesema hali ya afya ya mumewe inaridhisha baada ya kupatiwa matibabu ya muda mrefu.  “Namshukuru Mungu kwa rehema zake, kulikuwa na nyakati ngumu sana zilizojaa maumivu na majaribu, lakini leo hii mume wangu ni mzima, imara na ana afya njema,” alisema.

Hatahivyo, ameongezea  kutokana na hali ya afya ya mumewe kuendelea kuimarika basi matarajio yake mwaka 2026 ataraejea uraiani kwa shughuli zake za sanaa.SOMA: Prof Jay: DM yangu ina maombi mengi mno

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button