‘Ulevi tishio jipya kwa vijana’

DAR ES SALAAM; MAPAMBANO dhidi ya dawa za kulevya nchini yamepiga hatua kubwa kiasi cha kufan ya dawa hizo kutopati kana kirahisi mitaani.

Hata hivyo imeelezwa mafanikio hayo sasa yameambatana na changamoto mpya ya kuongezeka kwa ulevi wa pombe hususani miongoni mwa vijana.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam na Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo wakati wa kikao kazi kati ya mamlaka hiyo na waandishi wa habari.

Lyimo alisema juhuza pamoja kati ya DCEA, vyombo vya ulinzi na us alama pamoja na wananchi zimefanikisha kudhibiti kwa kiwango kikubwa biashara na matumizi ya dawa za kulevya, hali iliyosababisha dawa hizo kama heroini na kokeni kutokuwepo mitaani kama ilivyokuwa awali.

“Tanzania imefanya kazi kubwa kupunguza dawa za kulevya. Zamani zilikuwa zinauzwa hadharani hadi wafanyabiashara wake kuimbwa kwenye bendi za muziki lakini hali hiyo haipo tena,” alisema.

Aliongeza kuwa maneno yaliyokuwa yakitumika kuashiria biashara ya dawa za kulevya kama ‘zungu la unga’ hayasikiki tena, jambo linalothibitisha mafanikio ya mapambano hayo.

Hata hivyo, alisema kupungua kwa upati kanaji wa dawa za kulevya kumesababisha baadhi ya waliokuwa waraibu kuele keza matumizi yao kwenye pombe, hali inayochochea kuongezeka kwa ulevi wa kupindukia

“Kwa sasa vijana wengi wameingia kwenye ulevi wa pombe baada ya kukosekana kwa dawa za kulevya. DCEA ina vituo vya urekebu 78 nchini na kwa sehemu kubwa vime jaa waraibu wa pombe,” alisema Lyimo.

Alieleza kutokana na mafanikio ya kudhibiti dawa za kulevya, Tanza nia si mlango wa kupiti sha dawa hizo tena, hali iliyopunguza hata ukaguzi mkali kwa Watanzania wanaosafiri nje ya nchi kupitia viwanja vya ndege.

Lyimo alisisitiza kuwa sasa kuna haja ya kuele keza nguvu zaidi katika kudhibiti ulevi wa pombe, ambao umeanza kuathiri jamii kwa kasi, hasa vijana. Alihimiza watu wenye uraibu wa pombe kujitokeza na kujiunga na vituo vya urekebu ili kupata tiba na msaada wa kitaalamu.

Akizungumzia kikao kazi hicho, alisema DCEA inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya na changamoto mpya ya ulevi, akisisitiza kuwa waandishi wa habari ni wadau muhimu katika kuelimisha jamii na kub adili mitazamo hasi

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….

    This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com

  2. I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…

    This is what I do………………………………….. ­­­ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button