Dk Muyungi asihi vijana fursa muungano, mazingira

KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dk Richard Muyungi amewasihi vijana kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye masuala yanayohusiana na Muungano pamoja na Uhifadhi na Utunzaji wa mazingira ili kuleta maendeleo endelevu ya taifa.

Ameyazungumza hayo alipokutana na Taasisi ya vijana ya Green Samia Foundation, jijini Dar-es-salaam ambao wengi wao wanajihusisha na Uhifadhi na Utunzaji wa Mazingira na kueleza kuwa wanayonafasi kubwa ya kuchangamkia fursa zinazopatikana.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Richard Muyungi.

Amesema kuwa vijana wana nafasi kubwa ya kunufaika na fursa hizo kwa kushiriki katika masuala ya mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuanzisha shughuli za kiuchumi zinazolinda mazingira kama vile biashara ya kaboni.

Amesisitiza; “Muungano una unaleta umoja na ushirikiano kwa vijana, pamoja na kubuni na kutekeleza miradi ya kimazingira yenye manufaa kwa wananchi, ushiriki wao ni nguzo muhimu katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu”.

Naye Katibu wa taasisi ya Green Samia Foundation, Sarah Pima ameahidi kutoa ushirikiano katika shughuli na majukumu yote ya serikali yanayo husisha uhifadhi wa mazingira pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Ameomba msaada wa kitaalamu kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (upande wa mazingira) kwa ajili ya kutoa elimu kwa vijana kuhusu utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Dk Muyungi ametoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kuendelea kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mafunzo, rasilimali na na majukwaa ya ushiriki, ili kuongeza mchango wao katika uhifadhi wa mazingira kupitia masuala ya Muungano.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. The texture and color of this strongest THC Beer look entirely and cultured, with no cloudiness or residue. The cut off pours smoothly, and the cap seals tightly. Complete, it feels like a thoughtfully made product designed with quality in mind.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button