‘Ni mara ya kwanza kuandaa dira na mpango wakati mmoja’

DODOMA; SERIKALI imesema hii ni mara kwanza kwa nchi Tanzania kuandaa dira na mpango elekezi kwa wakati mmoja.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akiwasilisha nyenzo tatu zitakazowezesha kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Nyenzo hizo ni Mpango Elekezi wa Muda mrefu wa miaka 25 (2026/27 hadi 2050/51), Mpango wa Nne wa Maendeleo wa miaka mitano (2026/27 hadi 2030/31) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2026/27.
Amesema Tanzania ina historia ndefu ya kuandaa mipango ya maendeleo, ambapo mpango elekezi wa maendeleo wa muda mrefu wa kwanza uliandaliwa mwaka 1964, ukiwa ni wa kipindi cha miaka 16 (1964 – 1980).

“ Hata hivyo, Dira hii haikuanza kutekelezwa mapema kutokana na kutokuandaliwa mpango elekezi wa muda mrefu wa maendeleo ambao ulipaswa kutafsiri maono na matarajio yaliyokuwemo katika dira hiyo.

“Hali hii ilitokana na mashariti ya taasisi za kifedha duniani (IMF na Benki ya Dunia) ya kuitaka Tanzania kuandaa na kutekeleza mpango maalum wa kupunguza umaskini (MKUKUTA), ikiwa ni sehemu ya kukidhi masharti ya kukidhi vigezo yaliyowekwa kwa nchi maskini kusamehewa madeni chini ya mpango maalum wa nchi maskini zenye madeni makubwa (Heavily Indebted Poor Counties- HIPC).

“Mwaka 2010 Serikali ilifanya tathmini ya utekelezaji wa Dira 2025 na kubaini kuwa dira hiyo ilikuwa haijaanza kutekelezwa kikamilifu kama ilivyotarajiwa kutokana na kukosekana kwa mpango elekezi wa kuongoza utekelezaji wake.

“Kufuatia tathmini hiyo, Serikali iliandaa Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu wa kwanza (first Long-Term Perspective Plan – LTPP) wa miaka 15 (2011/12 – 2025/26), ulioandaliwa kwa ajili ya kuongoza utekelezaji Dira 2025 kwa miaka 15 iliyokuwa imebaki.

“Hivyo basi, hii ni mara kwanza kwa nchi yetu kuandaa dira na mpango elekezi kwa wakati mmoja. Hii inamaanisha kuwa hatuna sababu ya kuchelewa kuanza kutekeleza Dira 2050. Tunamshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa uongozi na maelekezo yake,” amesema.

“Mpango huu ulipangwa kutekelezwa kupitia mipango ya muda wa kati mitatu: I: 1964-1969; II: 1969 – 1974; na III: 1975 – 1980.

“Hata hivyo, mipango hii haikutekelezwa kikamilifu kutokana na changamoto za kiuchumi zilizoikumba dunia na nchi yetu, ikiwemo ukame na hali mbaya ya hewa, kuharibika kwa soko la mafuta duniani, na vita kati ya Tanzania na Uganda ya 1978/79. Kutokana na changamoto hizi, utekelezwaji wa mpango elekezi ulisitishwa rasmi mwaka 1976,” amesema Waziri Mkumbo.

“Mwaka 1981 Serikali iliandaa mpango elekezi wa maendeleo wa muda mrefu wa pili wa miaka 20 (1981 – 2000). Mpango huu ulipangwa kutekelezwa kupitia mipango ya muda wa kati minne.

“Hata hivyo, mpango huu nao haukutekelezwa kikamilifu kutokana na majanga ya kiuchumi yaliyoendelea kuikumba dunia katika miaka ya 1970 na 1980, hali iliyolazimisha nchi yetu kujielekeza kutekeleza mipango ya muda mfupi na ya dharura.

“Katika kipindi hiki, mipango ya muda mfupi na ya dharura iliyotekelezwa ni pamoja na Programu ya Kitaifa ya Kujihami Kiuchumi (National Economic Survival Programme – NESP) iliyotekelezwa mwaka 1981 – 1982; Programu za Kurekebisha Uchumi (Structural Adjustment Programmes-SAPS) zilizotekelezwa mwaka 1983 – 1985; na Programu za Kufufua Uchumi (Economic Recovery Programme – ERPs) zilizotekelezwa 1986 – 1995,” amesema.

“Kutokana na maelezo ya hapo juu, Tanzania haikuwahi kutekeleza kikamilifu mpango wa maendeleo wa muda mrefu hadi mwaka 2000 ilipozindua dira ya kwanza ya Taifa ya maendeleo (Dira 2025).

“ Hata hivyo, Dira hii haikuanza kutekelezwa mapema kutokana na kutokuandaliwa mpango elekezi wa muda mrefu wa maendeleo ambao ulipaswa kutafsiri maono na matarajio yaliyokuwemo katika dira hiyo.

“Hali hii ilitokana na mashariti ya taasisi za kifedha duniani (IMF na Benki ya Dunia) ya kuitaka Tanzania kuandaa na kutekeleza mpango maalum wa kupunguza umaskini (MKUKUTA), ikiwa ni sehemu ya kukidhi masharti ya kukidhi vigezo yaliyowekwa kwa nchi maskini kusamehewa madeni chini ya mpango maalum wa nchi maskini zenye madeni makubwa (Heavily Indebted Poor Counties- HIPC).

“Mwaka 2010 Serikali ilifanya tathmini ya utekelezaji wa Dira 2025 na kubaini kuwa dira hiyo ilikuwa haijaanza kutekelezwa kikamilifu kama ilivyotarajiwa kutokana na kukosekana kwa mpango elekezi wa kuongoza utekelezaji wake.

“Kufuatia tathmini hiyo, Serikali iliandaa Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu wa kwanza (first Long-Term Perspective Plan – LTPP) wa miaka 15 (2011/12 – 2025/26), ulioandaliwa kwa ajili ya kuongoza utekelezaji Dira 2025 kwa miaka 15 iliyokuwa imebaki,”

“Hivyo basi, hii ni mara kwanza kwa nchi yetu kuandaa dira na mpango elekezi kwa wakati mmoja. Hii inamaanisha kuwa hatuna sababu ya kuchelewa kuanza kutekeleza Dira 2050. Tunamshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa uongozi na maelekezo yake,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button