Dhima ya Mpango ukuaji uchumi, ajira

DODOMA; SERIKALI imesema Dhima ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/27 – 2030/31 ni mageuzi kwa ajili ya ukuaji wa uchumi jumuishi nau wa ajira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof Kitila Mkumbo, ametoa kauli hiyo bungeni leo akiwasilisha nyenzo tatu zitakazowezesha kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Nyenzo hizo ni Mpango Elekezi wa Muda mrefu wa miaka 25 (2026/27 hadi 2050/51), Mpango wa Nne wa Maendeleo wa miaka mitano (2026/27 hadi 2030/31) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2026/27.

“hima hii inaelekeza kuweka msukumo wa kipekee katika kutekeleza mageuzi makubwa yatakayobadilisha mifumo, mitazamo na 10 mwenendo katika utendaji ili kuchochea tija katika uzalishaji, kuongeza uwezo wa nchi katika kushindana kikanda na kimataifa, na kuchochea muunganiko wa sekta mbalimbali.

“Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, viwanda na biashara katika ukanda wa Afrika,” amesema Waziri Mkumbo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button