Dk Nchimbi ahadharisha kutonesha vidonda vya vurugu za Oktoba 29

MAKAMU wa Rais, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema si vyema kwa viongozi wa serikali, asasi za kijamii, viongozi wa vyama vya siasa na wanaharakati kuzungumzia yaliyojiri Oktoba 29, mwaka jana nje ya mfumo wa kisheria.

Dk Nchimbi alisema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria na kuzinduliwa kwa mwaka mpya wa shughuli za kimahakama kwa mwaka 2026 Dodoma.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameshaunda Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu 2025 ili kushughulikia suala hilo.

“Namshukuru Rais wa TLS ametuasa viongozi, kuwa si vizuri kuendelea kuzungumzia yaliyojiri Oktoba 29 kwa sababu yanatonesha vidonda na pengine yanaweza yasisaidie sana katika mchakato wa haki, kwanza nakubaliana naye kwa asilimia 100,” alisema Dk Nchimbi.

Aliongeza: “Niongeze pale aliposahau, kwamba si viongozi wa serikali pekee na viongozi wa vyama vya siasa, taasisi za kijamii na wanaharakati. Rais (Samia) ameunda Tume inaendelea kufanya kazi, kuendelea kuzungumza nje ya mfumo wa kisheria uliowekwa kwa jambo hili ni kutolitendea haki taifa letu”.

Dk Nchimbi alisema ni muhimu kwa kila mtu anayeipenda Tanzania akubaliane na Rais wa TLS watu wasitoneshane na watoe nafasi kwa vyombo vya kisheria kutimiza wajibu wake.

Pia, aliipongeza TLS kwa kutoa mchango mkubwa na kwa kushirikiana kikamilifu na Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na taasisi nyingine katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za uwakili.

“Napenda kuwahakikishia kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa TLS na wadau wengine wote wa
haki ili kufikisha huduma za kisheria kwa wananchi kwa wakati na kwa ufanisi,” alisema.

Habari Zifananazo

12 Comments

  1. I’m really impressed with your writing skills as well as with the layout on your blog.
    Is this a paid theme or did you customize it yourself? Anyway keep
    up the nice quality writing, it is rare to see a nice blog like this one these days.

  2. Hi! I know this is somewhat off topic but I was wondering which blog
    platform are you using for this site? I’m getting tired of WordPress
    because I’ve had issues with hackers and I’m looking at alternatives
    for another platform. I would be great if you could point me in the direction of a good platform.

  3. Hi there everyone, it’s my first visit at this web page, and post is actually fruitful for me, keep up posting these
    types of articles.

  4. Good day! This is kind of off topic but I need some help from an established blog.
    Is it very hard to set up your own blog? I’m not very techincal but I can figure things out pretty fast.
    I’m thinking about setting up my own but I’m not sure where to start.
    Do you have any points or suggestions? With thanks

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button