Tahadhari ichukuliwe mvua za masika kupunguza athari

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa masika unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa Februari hadi Mei kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka.

Katika taarifa yake, TMA imetabiri matarajio ya mvua za wastani hadi juu ya wastani kwa maeneo mengi ya Pwani ya Kaskazini na baadhi ya maeneo ya Magharibi mwa ukanda wa Ziwa Victoria.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a alisema Dar es Salaam hivi karibuni kuwa matarajio ni mvua za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki na baadhi ya maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria.

Hata hivyo, aliweka wazi kuwa matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo vipindi vya mvua kubwa yanaweza kujitokeza hata katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.

SOMA: Hali ya hewa yaonya ongezeko la mvua

Maeneo yaliotajwa ni mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga, maeneo ya Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, visiwa vya Unguja na Pemba na Ukanda wa Ziwa Victoria katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara na maeneo ya Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya Februari na ya kwanza ya Machi, 2026 kwa maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria na wiki ya pili na ya tatu ya Machi kwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini na kwamba ongezeko la mvua linatarajiwa Aprili.

Kama TMA ilivyotoa tahadhari kwamba hata katika maeneo yenye mvua chini ya wastani zinaweza kupata mvua nyingi hivyo tunasisitiza Watanzania kufuatilia kwa karibu taarifa za TMA kila siku ili kuchukua hatua za kudhibiti athari mbaya hasa mafuriko na uharibifu wa mali yakiwemo mazao hasa kwa mikoa yote inayopata mvua za masika.

Pia tahadhari ichukuliwe ya upungufu wa maji kwa maeneo yatakayopokea mvua za wastani hadi chini ya wastani na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafuzi wa maji.

Wakulima wawe macho kuhakikisha mazao shambani yanakuwa salama kwa kutengeneza mitaro na kutoharibu miundombinu ya kusafirisha maji.

Hali kadhalika wafanyabiashara na wananchi wote wazingatie usafi wa mazingira kuzuia magonjwa ya mlipuko.

Serikali izidi kutoa elimu kwa jamii kuwalinda watoto wanaokwenda shule ili wasivuke kwenye maji yanayotembea kwa kasi kwani ni hatari kusombwa na kupoteza maisha.

Tunazikumbusha mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha mitaro ya maji taka inakuwa katika ubora kuruhusu maji kupita badala ya kukimbilia kwenye makazi ya watu na kusababisha mafuriko.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do……………………………………………………………………………………………………………….  www.join.work27.com 

  2. Start working at home with Google! It’s by-far the best job I’ve had. Last Wednesday I got a getting a check for $19400 this – 4 weeks past. I began this 8-months ago and immediately was bringing home at least $220 per hour. I work through this link, go to tech tab for work detail..

    Open This Website——≻≻≻≻≻www.hot.cash54.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button