Serikali yaendelea kuimarisha miradi Dar

DAR ES SALAAM: Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha uchumi wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert John Chalamila, amefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mivumoni iliyopo Wilaya ya Kinondoni.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Chalamila amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo, kuongeza thamani ya ardhi na nyumba pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.
Amesema miradi ya miundombinu ni nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo ya wananchi na kuondoa changamoto za muda mrefu zinazohusiana na usafiri, hususan nyakati za mvua.
Chalamila amewataka wananchi wa Kinondoni kuwa mabalozi wa maendeleo kwa kujituma na kutumia fursa zinazotokana na utekelezaji wa miradi hiyo badala ya kupoteza muda kwenye mambo yasiyo na tija.
“Niwaombe tukawe mabalozi wazuri kwa nafsi zetu wenyewe kabla hujawa balozi mzuri wa serikali… Rais anatamani kila mtu awe na hela mfukoni,” amesema.
Amesema kukosekana kwa kipato na malengo kwa baadhi ya vijana kunasababisha kujihusisha na umbea na msongo wa mawazo, hali inayopunguza uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kujiletea maendeleo.
“Umbea uliokomaa unatokana na ukosefu wa pesa mfukoni,” amesema.
Aidha, amewahimiza vijana kutumia fursa zinazotokana na ujenzi wa barabara hiyo ikiwemo ajira za muda na biashara ndogondogo zitakazowanufaisha kabla na baada ya mradi kukamilika.
Katika hatua nyingine, Chalamila amewataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili wananchi waanze kunufaika mapema na huduma hiyo muhimu.
Amesema serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo ili kuhakikisha inaleta tija na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi.




I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com