Kilo 900 za mahindi zakabidhiwa Liwelyangula

SHINYANGA: WANAWAKE manispaa ya Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo kilo 900 za mahidi na sukari kilo 145 katika shule ya msingi Liwelyangula.

Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO Gerald Ng’ong’a kwa niaba ya wadau waliochangia vyakula hivyo ikiwa amezindua rasmi upatikanaji wa chakula kwenye shule hiyo huku akieleza kutoa kilo 100 za mahindi kila baada ya miezi mitatu.

Ngo’ng’a amesema wazazi wanatakiwa kuunga mkono juhudi hizi kwa kuchangia chakula na mikakati iwepo ya kila robo na utaratibu wa utumikaji wa vyakula shuleni hapo walimu washirikishe wanafunzi waone vimetumikaje.

“Leo linafanyika zoezi la uzinduzi rasmi wa chakula shule ya msingi Liwelyangula wazazi nasi tuchangie libaki jukumu la walimu kufundisha na watoto wetu wafaulu mitihani yao”amesema ng’ong’a.

Mwakilishi kutoka shirika la Invest in Children Society (ICS) linalojihusisha na masuala ya malezi na makuzi ya mtoto Lucy Maganga akieleza suala la mawasiliano amesema wazazi wengi wanakosa kuwa na mawasiliano mazuri na watoto hilo ndio gepu kubwa ambalo pia kushindwa kujua mahitaji muhimu ya shule

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Liwelyangula Lea Mzava amesema shule hiyo ina wanafunzi 452 na leo amefurahi maadhimisho ya siku ya wanawake na uzinduzi rasmi wa chakula shuleni hapa lengo lilikuwa kuhamasisha wazazi kuchangia chakula kwani robo ya wanafunzi ndiyo wamekuwa wakilipiwa chakula.

Mwenyekiti kamati ya shule Machibya James amesema kwenye vikao wamekuwa wakisisitiza wazazi kuchangia na sasa wanakuka na mpango mpya mzazi asiyechangia chakula atachukuliwa hatua.

Ofisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga Nyanjura Kiyenze amesema wazazi upo umuhimu wa utoaji chakula shuleni wasipo kula shuleni ni chanzo cha kufanya vibaya darasani igeni mfano wa shule ya msingi Lubaga wazazi wanatoa chakula na wanafunzi wanafanya vizuri.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button