‘Matumizi ya Kiswahili sekondari yanajitaji tafiti za kina’

MWANZA: KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi amesema wazo la kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia kuanzia shule za msingi hadi sekondari ni zuri, lakini utekelezaji wake unahitaji tafiti za kina ili kuhakikisha wataalamu wa Tanzania wanaendelea kushindana kimataifa.

Kihongosi ameyasema hayo leo Machi 11,2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa shina namba 20 Tawi la Kanyamwanza Kata ya Mwabaruhi wilayani Sengerema mkoani Mwanza alipotembelea na kushiriki kikao cha shina hilo, ikiwa ni muendelezonwa ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Kihongosi amezungumza hayo kijibu hoja ya Mwenyekiti wa shina hilo, Nabor Kavishe walipoomba Kiswahili kifundishwe katika ngazi zote za elimu kuanzia msingi hadi sekondari ili kuiendeleza tunu hiyo kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazojifunza kupitia lugha zao.

Akijibu hoja hiyo Kihongosi amesema Kiswahili ni moja ya tunu muhimu za taifa na kinapaswa kuenziwa, lakini ulimwengu wa sasa wa sayansi, teknolojia na taaluma mbalimbali bado unatumia zaidi lugha ya Kiingereza, hali inayohitaji kuangaliwa kwa umakini kabla ya kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu.

“Ni jambo jema kutumia Kiswahili katika kufundishia kwa sababu ni lugha yetu ya taifa. Hata hivyo, dunia ya sasa inatumia zaidi Kiingereza katika sayansi na teknolojia, hivyo suala hili linahitaji tafiti zaidi ili kuhakikisha wataalamu wetu wanaweza kushindana kimataifa,” amesema Kihongosi.

Amefafanua kuwa katika baadhi ya taaluma kama udaktari, vifaa na teknolojia nyingi za hospitali hutumia lugha ya Kiingereza, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuangalia kwa makini namna bora ya kusawazisha matumizi ya lugha hizo katika elimu.

Awali, Akisoma taarifa ya shina hilo Kavishe amesema shina hilo lina jumla ya wanachama 140 lakini waliohai ni 122 na ambao sio hai ninwanachama 18 pekee na uhai w achama chao unaendelea vizuri.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am making a good salary from home $4580-$5240/week , which is amazing und­er a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now its my duty to pay it forward and share it with Everyone,
    .

    Here is I started______________ e­­­a­­­r­­­n­­­s­­­m­­­a­­­r­­­t­­­w­­­i­­­t­­­h­­­u­­­s­­­.­­­n­­­e­­­t­­­l­­­i­­­f­­­y­­­.­­­a­­­p­­­p­­­

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button