Serikali yatoa maagizo 8 utendaji kampuni zake

SERIKALI imetoa maagizo manane kuimarisha utendaji wa kampuni ambazo ina umiliki wa hisa ndogo ikiwa ni se hemu ya jitihada za kufi kia uchumi wa kipato cha juu cha kati kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Mpango huo unalenga kukuza uchumi wa Tanzania kutoka Dola za Marekani bilioni 85 za sasa hadi Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, jambo linalohitaji ufanisi mkubwa wa uwekezaji wa umma hususani katika kampuni hizo.

Akifungua Mkutano wa siku tatu wa Wakurugenzi wa Kampuni zenye Hisa Ndogo unafanyika jijini Arusha ukiwa na kaulimbiu: ‘Kutoka Ufuatiliaji wa Kawaida hadi Uongozi wa Kimkakati unaotazama mbele’, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar alisema maagizo hayo yanalenga kuimarisha uendeshaji wa kampuni kwa uwazi, ufanisi na faida, huku zikichangia kikamilifu mageuzi ya uchumi.

Alisisitiza bodi za wakuru genzi na menejimenti kuoainisha mikakati yao na vipaumbele vya maendeleo ya taifa pamoja na mwelekeo wa uchumi wa dunia.

Aidha, ameziagiza kampuni kutumia teknolojia kuimarisha uwazi, kujenga imani kwa umma na kuboresha mifumo ya utawala huku akisisitiza umuhimu wa uongozi unaotaza ma mbele ili kutambua hatari na fursa mapema.

Alisema serikali pia imehi miza ushirikiano na ubia kati ya kampuni ili kuongeza ufanisi, kubadilishana uzoefu na kufun gua fursa mpya za kiuchumi ikiwamo mifumo madhubuti ya utawala inayozingatia uwajibi kaji, uwazi na maadili, na matu mizi ya mikakati ya kuongeza ufanisi na faida kwa wanahisa na serikali.

Aliongeza kuwa uchambuzi wa taarifa za kiuchumi na ush indani ni muhimu ili maamuzi yafanywe kwa takwimu sahihi, hatua itakayoongeza uzalishaji na ushindani katika masoko ya ndani na nje.

Kupitia Dira 2050, serikali inalenga kuongeza mchango wa mapato yasiyo ya kodi kutoka asilimia tatu hadi 10 ndani ya miaka mitano, sawa na Sh tril ioni tano kwa mwaka.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha alisisitiza kuwa mafanikio hayo yanahitaji mabadiliko ya fikra na mbinu za kazi kuelekea uongozi unaozingatia ubunifu, utabiri na wepesi wa kubadilika.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais anayeshughulikia Uwekez aji, Dk Fred Msemwa alisema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kui marisha sekta binafsi, akisisitiza kuwa ni mhimili muhimu wa kufanikisha Dira 2050.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alisema mkutano huo ulioanza mwaka 2024 ni jukwaa muhimu la kujadili utawala na utendaji wa kampuni hizo.

Aliongeza kuwa katika miaka mitano iliyopita, uwekezaji wa serikali katika kampuni hizo umeongezeka kutoka Sh bilioni 821 hadi Sh trilioni 3.6, huku gawio likikua kwa asilimia 357 kutoka Sh bilioni 58 hadi Sh bilioni 266.

Mkutano wa MIF 2026 ume wakutanisha washiriki wapatao 200 kujadili namna ya kuboresha utendaji na utawala wa kampuni hizo ili kuchangia zaidi maende leo endelevu ya taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button