Chuo chahamasisha maadili kwa vijana

BABATI: Waumini wa Dini ya Kiislamu Wilaya ya Babati mkoani Manyara wamesema kufunguliwa kwa chuo cha kiislamu cha malezi bora ya maadili kwa vijana kitasaidia kukuza ari ya kumcha Mungu kujenga maadili yatakayosaidia kudumisha amani na utulivu.
Pia kurekebisha tabia zisizofaa kwa jamii ikiwemo uvunjifu wa amani na ukatili wa kijinsia.
Hayo yameelezwa Aprili 12, 2026 katika ufunguzi wa Chuo cha Kiislam cha Darul Ulum Wal Adab kilichopo Maisaka A Katani Wilaya ya Babati mkoani Manyara.
Naibu Imamu Masjidi Rahma Msikiti Mkuu, Radawi Athumani amesema chuo kitasaidia katika malezi ya vijana kimaadili ili wawe wacha Mungu na raia wema.
”Hii ni nyumba iliyoandaliwa kwa ajili ya elimu na adabu tunatarajia vijana wetu kupata elimu,adabu na maadili tunayotaka tuyashi katika jamii,” amesisitiza.
Kumekuwepo na mmomonyoko wa maadili katika jamii hasa kwa vijana amesema jambo ambalo dini ya kiislamu hukemea na kusimamia misingi ya kumcha Mwenyezi Mungu na kuwa na tabia njema ambapo ni miongoni mwa maadili na kuwa na adabu njema.
Mkuu wa chuo cha Darul Ulum Wal Adabu Abdulkarim Yusuph Shabani amebainisha kwamba bado kuna uhitaji wa kuendeleza majengo ya chuo kwa sasa chuo kina ofisi, madarasa mawili na mabweni mawili ya vijana wa kiume ambapo hayatoshelezi.
” Tunawatia watu wa kheri sisi hatuna mfadhili maalum kwamba huyu ndiye anatusaidia hapana, watu wa kheri wake kuwekeza Sehemu ambayo itawasaidia sana siku ya kiama,”amesema Shabani.
Naye, Katibu Bakwata Mkoa wa Manyara, Alhaj Ahmadi Khairallah ameeleza Bakwata imeridhia chuo hicho kusimamia vizuri malezi bora na maadili ya dini kwa waislamu wote na kuwashauri waislamu kuendelea kuwekeza katika ujenzi wa vyuo na madrasa mbalimbali ili kupata vijana na viongozi wenye maadili.mema katika kumuogopa Mungu.
Feisal Athumani mwanafunzi wa chuo cha Darul Ulum Wal Adab na Mwajuma Hussein mkazi wa eneo la Maisaka A Katani wamebainisha kwamba uwepo wa chuo hicho utasaidia kupunguza migogoro ya ndoa na kurejesha amani na utulivu katika familia.
Jiwe la msingi la chuo hicho limewekwa na Alhabib Sayyidi Jaffar Swadiq Bin Alhabib Dhaifu Muhamadi Bin Sharifa Said Albiydhi kutoka Malindi Kenya akiwa na Mudiru wa maahadi Hayatil Islamiya Sheikh wa mkoa wa Manyara Alhaji Muhammad Kadidi Aprili 15, 2025.



Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site