Ecobank yaahidi kuongeza uwekezaji Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na uongozi wa Benki ya Ecobank, ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Biashara na Uwekezaji kutoka makao makuu ya benki hiyo nchini Togo, Bw. Michael Larbie, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank Tanzania, Ndugu Charles Asiedu.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 15 Aprili 2026, Ikulu Zanzibar, ambapo pande zote mbili zimejadili masuala ya ushirikiano wa kiuchumi na fursa za uwekezaji. Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Ecobank kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi.

Aidha, ameihakikishia benki hiyo ushirikiano endelevu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku akibainisha fursa mbalimbali za uwekezaji zikiwemo bandari, miundombinu ya barabara na uchumi wa buluu.Kwa upande wake,Michael Larbie amesema Ecobank itaendelea kushirikiana na Zanzibar na kuimarisha ushirikiano wa kifedha na kibiashara barani Afrika kupitia mpango wake wa Pan African Partnership. SOMA: Samia, Mwinyi kuongoza kumbukizi ya Karume leo





Habari Leo Mko Fire🔥 ajirazote.co.tz
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸www.work27.online