Serikali yataja mbinu kuondoa migogoro kazini

MOROGORO: SERIKALI kupitia Ofisi ya Kamishna wa kazi imevitaka vyama vya wafanyakazi nchini kufanya maamuzi muhimu kwa njia ya ushirikishaji kwa wananchama wao ili kuondokana na migogoro isiyo ya lazima.

Kamishna wa kazi Msaidizi ,Emmanuel Mweta amesema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa 32 wa Baraza kuu la Chama cha Wafanyakazi Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) mjini Morogoro.

Mweta amesema pamoja na Serikali kuendelea kufanyia kazi mapungufu na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika vyama vya wafanyakazi , bado nafasi ya vyama vya wafanyakazi inabaki kuwa muhimu, hususan kupitia majadiliano ya pamoja kati ya vyama, waajiri na wafanyakazi katika sekta mbalimbali

“Nasisitiza kwa Vyama vya Wafanyakazi nchini  kuendelea kuimarisha mahusiano bora kazini ili kuendeleza  ustawi kazini” amesema Mweta.

Kamishna wa Kazi Msaidizi huyo amesema  hatua hiyo itaweza kuepusha migogoro inayoweza kupoteza mahusiano kazini na  pia inaweza kupoteza muda katika kusuruhisha migogoro badala ya kufanyakazi ili kujiletea maendeleo.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa TUICO Taifa, Abdallah Msese amesema mkutano mkuu  huo uliambatana  na semina maalum kwa Wajumbe wa Baraza Kuu, ikiwa na mada muhimu zinazogusa maendeleo ya wafanyakazi na vyama vyao, uongozi katika Vyama vya Wafanyakazi, Afya ya Akili, Wosia na Mirathi.

Amesema katika mkutano mkuu wajumbe wamejadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi ikiwemo za waajiri kutozingatia utekelezaji wa kiwango cha chini cha mishahara hasa katika sekta binafsi.

Msese amesema pamoja na mafanikio ambayo Chama kimeyapata bado kinapitia changamoto mbalimbali zikiwemo za baadhi ya Waajiri wakorofi kutoruhusu Watendaji wa Chama kutekeleza majukumu yao mahala pa kazi.

Pia baadhi ya Waajiri kushindwa kuzingatia ulipaji wa mishahara kama ilivyoanishwa wazi kwenye amri ya kima cha chini cha mishahara hasa katika sekta binafsi.

Kwa upende wake Mkuu wa Idara ya Sheria TUICO ,Wakili Noel Nchimbi,  amesema Chama kinaendelea kutoa elimu kwa wafanyakazi na waajiri katika mabadiliko mbalimbali ya kisheria na sera ili kukabiliana na changamoto na migogoro inayojitokeza mahala pa kazi.

“ Utoaji wa elimu hizo umesaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza migogoro kwa njia ya usuruhishi kama muongozo ya kisheria inavyo taka badala ya kuwa na kesi ambazo zingeweza kutumia muda mwingi kwenye vyombo vya kisheria” amesema Wakili Nchimbi.

Wakili Nchimbi amesema katIka sera kwenye utatuzi wa migogoro , Chama kinatumia zaidi suala la usuruhishi.

“ Sisi kama chama tumefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 98 katika usuruhishi maana kwa mwaka jana  (2025) peke yake tumeweza kusuruhisha migogoro 94 ambayo kama ingeenda mahakamani watu wangetumia muda mwingi zaidi” amesema Wakili Nchimbi.

Katika hatua nyingine TUICO imezindua kitabu cha mafunzo kwa wafanyakazi kijulikanacho “Elimu ya Fedha na Uchumi kwa Wafanyakazi” ambacho kinalenga kuwajengea uwezo katika usimamizi wa fedha na ustawi wa kiuchumi.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she kaz convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website

    HERE——— http://www.giftpay7.vip

  2. start making over $600 a day from yodtimeshare home. I made $18,781 from this job in my spare time after college. *a11 easy wdork and his sdteady income is amazing. No skills are required for this job. All you need to know is how to copy and padste items online. Sign up today by following the details on this page.

    Here is I started.….w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

  3. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button