Tanga yajipanga uchumi wa kijani

TANGA: MKUU wa Mkoa wa Tanga, Balozi Bk Batilda Burian amesema mkoa utaendelea na jukumu la kusimamia uhifadhi wa mazingira ,vyanzo vya maji ,ulinzi na utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhakikisha kila mwaka halmashauri zake zinapanda miti 1,500,000.

Dk Burian amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), ofisini kwake mjini humo.

Amesema sio tu kupanda miti bali ni pamoja na kuangalia vyanzo vya maji na kwenye maeneo yote ambayo yanatakiwa kulindwa na kuhakikisha shughuli zote zinazofanyika zinakuwa rafiki wa mazingira.

“Tunapotaka maendeleo endelevu ni lazima tuiangalie nguzo za kiuchumi, kisisasa, kijamii na pia ya kimazingira “ na bila ya kuwa na uwiano huo wa pamoja tunaweza kufika mahali kama taifa tukaweza kupata madhara,”amesema Dk Burian.

Dk Burian alisema mkoa huo umeanza mchakati mkubwa wa upandaji wa miti hasa ya matunda ikiwemo miembe, minazi na mikarafuu hasa katika wilaya ya Muheza na Mkinga ambapo kwa sasa  ni kati ya mikoa unaiozalisha karafuu ukiondoa Zanzibar, Pemba na Morogoro.

Amesema mchakato huo unalenga kupanda miti milioni mbili katika kipindi cha miaka miwili na kwa msimu wa mwaka huu  mkoa umelenga kupanda miti 10,000 na mingine itakayopandwa kokoa na korosho pamoja na miti ya mbao.

Mkuu wa mkoa huo amesema endapo wananchi wakijua miti wanayoipanda inakwenda kusaidia maisha yao ya kiuchumi kutakuwepo na mwitikio mkubwa zaidi .

Dk Burian pia amesema mkoa huo unasajili miradi ya hewa ukaa na hadi sasa imesajiliwa miradi minne katika wilaya ya Kilindi, Mkinga, Muheza na halmashauri ya Bumbuli wilaya ya Lushoto.

“Miradi hii ipo katika hatua mbalimbali ya kupata usajili  kwa ajili ya kupata hewa ya ukaa, wananchi wakichaona faida watatunza mazingira na misitu na hili limeleta msukumo kwa kila halmashauri kutaka kuanza miradi hii,”amesema Dk Burian.

Licha ya hayo amesemabado kunachangamoto nyingi na elimui inaendelea kutolewa kwa wananchi ili kuleta fursa kubwa kwa wageni na wataalamu waa TFS kwa kushirikiana kwenye uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Mkuu wa mkoa amesema jambo ambalo bado linaathiri ni suala la mkaa na kwamba Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekuwa ni championi wa masuala mazima ya nishati safu na kwa kuitikia hilo, mkoa umeshagawa majiko zaidi ya 20,000 na zoezi hilo linaendelea .

Pia amesema taasisi zote zikiwemo Magereza na shule za bweni zimeshaelekezwa kutumia majiko safi yanayotuimia nishati mbadala  badala ya kuni na mkaa.

“ Tumeweka katazo la kukata miti hata ukiwwa kwenye shamba lako lazima kupata kibali  na tumewaelekeza wakuu wa wilaya ndiyo wenye kutia kibali hiki na tumeshaelekezana,”amesema Dk Burian.

Dk Burian amesema kuwa Serikali ya mkoa pamoja na TFS wataendelea kusimamia na lengo ni kuhakikisha kwamba suala hilo la mkaa halitatumika kwa ajili ya kulipa faini na mtu aendelee bali tunataka kuzuia kabla haijakatwa.

“Ukishamkuta mtu emebeba mkaa ameshaharibu miti mingine ambayo ni ya asili inayoyumia miaka 50 hadi 100 kuota na hilo tumeliona tulisimamie kwa kushirikisha askari wa jeshi la akiba katika maeneo ya vijijini kugakikisha wanazuia ukataji huu wa miti na kushirikisha watendaji wa vijiji,”amesema

Amesema bado hatujafikia pale tunapohitaji kufika isipo kuwa juhudi hizo zinaendelea kusimamia kuhakikisha kwamba watu wanabadirika na kujua umuhimu na madhara ya kuharibu mazingira na faida ya kutunza mazingira .

“Nia yetu ni kuhakikisha kuona Tanga inakuwa ya Kijani,”amesema Dk Burian.

 

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. Start now generating extra home based cash by doing very easy and simple job from home. Last month i have earned $19753 from this job in my part time. This job is just awesome and its earning are greater than 9 to 5 office job. Join this right now by follow instructions here…

    >>>>>>>>>> http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button