FCS, UNICEF kuimarisha uwezo asasi za kiraia Tanzania

TAASISI ya Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania imezindua mradi ya kuimarisha uwezo inayolenga mashirika ya kiraia yanayoongozwa na vijana na wanawake katika mikoa mitatu muhimu ya Tanzania; Dar es Salaam, Zanzibar na Songwe.

Mradi huu ni wa kihistoria, ukiwa ni ushirikiano wa moja kwa moja kati ya FCS na Umoja wa mataifa, na hatua muhimu katika juhudi za pamoja za kuleta suluhisho zinazolenga watoto na vijana walio katika mazingira hatarishi nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kiongozi kutoka UNICEF, Miranda Armstrong alisema, “Kwa kuwekeza katika uwezo wa muda mrefu wa mashirika yanayoongozwa na vijana na wanawake, mradi huu unawawezesha asasi za kiraia kuwa na uimara wa kitaasisi na kimipango unaohitajika ili kuendelea kustawi hata baada ya ufadhili wa wadau kukamilika.”

Aidha, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ms Given Sure alisema, “Kuimarisha uwezo wa mashirika yanayoongozwa na vijana na wasichana/ wanawake kunaendana moja kwa moja na vipaumbele vya kitaifa vya Tanzania.

Hii inaunga mkono dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 kwa kukuza maendeleo jumuishi na uwezeshaji wa wananchi, na pia inaendeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (NPA-VAWC II) kwa kuimarisha juhudi za jamii katika kuzuia na kukabiliana na ukatili.”

Tanzania ina idadi kubwa ya vijana, ambapo takribani asilimia 23 ya watu wote ni balehe wenye umri wa miaka 10 hadi 19. Muundo huu wa idadi ya watu unaleta fursa na changamoto.

Vijana wana uwezo mkubwa wa kuchochea ubunifu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, lakini pia wanakabiliwa na hatari mbalimbali zinazohitaji hatua za haraka, shirikishi na zinazoendana na muktadha.

Changamoto hizo ni pamoja na viwango vya juu vya mimba za utotoni, ndoa za utotoni, na ukatili wa kimwili, kihisia au kingono, pamoja na upatikanaji mdogo wa huduma za afya na kijamii zinazowajali vijana, na nafasi finyu za kushiriki katika maamuzi yanayoat hiri maisha yao.

Mashirika ya kiraia yanayoongozw a na vijana na wanawake yako katika nafasi nzuri ya kushughulikia changamoto hizi. Yakiwa karibu na jamii, yana uelewa wa muktadha, imani ya jamii, na uwezo wa kuchukua hatua kwa haraka. Yanachangia kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa huduma, utetezi, ubunifu, na kuhakikisha uwajibikaji.

Baada ya mchakato wa maombi ya mwaliko maalumu, mashirika 30 kutoka Dar es Salaam, Zanzibar na Songwe yamechaguliw a. Mashirika haya yatapatiwa mafunzo maalum, ushauri elekezi (mentorship), na msaada wa kitaasisi ili kuimarisha utawala, uongozi, utetezi, usimamizi wa fedha, na uhamasishaji wa rasilimali.

Mashirika yatakayofaniki wa kukamilisha mafunzo na ushauri huo yataalikwa kuomba ruzuku ya awali ya Sh milioni 25 za Kitanzania kila moja, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya majaribio.

Foundation for Civil Society (FCS) ni taasisi inayoongoza nchini Tanzania katika utoaji wa ruzuku, inayolenga kuimarisha mashirika ya kiraia. FCS inasaidia mashirika yanayoongozwa na vijana, wanawake, na yale ya ngazi ya jamii kuwa na ufanisi zaidi, uwajibikaji, na uendelevu katika kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Xổ số kiến thiết An Giang được quay thưởng định kỳ 2 lần mỗi tuần, vào Thứ Ba và Thứ Sáu, mang đến cơ hội trúng thưởng hấp dẫn và minh bạch cho người tham gia.
    Công ty TNHH MTV Xổ số Kiến Thiết An Giang
    📍 Địa chỉ: Số 1 Lê Lợi, Phường Mỹ Bình, TP. Long Xuyên, Tỉnh An Giang
    Với uy tín lâu năm, công ty không chỉ tổ chức quay số công khai, minh bạch mà còn đóng góp tích cực vào các hoạt động phúc lợi xã hội và phát triển địa phương.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button