RC Geita awaonya wanaokwamisha watumishi kubadili kada

GEITA: MKUU wa mkoa wa Geita, Martine Shigela amekemea tabia ya waajiri hususani maofisa utumishi wa ofisi za umma kukwamisha watumishi kubadilisha kada na kupandishwa madaraja.

Shigela ametoa kauli hiyo katika maazimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi, 2026) ambayo kimkoa yalifanyika katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro wilayani Geita.

Amesema kazi ya upandishaji madaraja ni endelevu na hivo maofisa utumishi mara kwa mara wanapaswa kupeleka taarifa za watumishi wanaohitaji kupandishwa madaraja kwa hatua zaidi.

“Nielekeze na kumkumbusha RAS (Katibu Tawala wa Mkoa) jambo hili tuendelee kulifuatilia kwa ukaribu, ili kila mfanyakazi anayestahili kupandishwa daraja aweze kupandishwa”, amesema.

Shigela amesema serikali haitakubali kuona watumishi wa umma waliojiendeleza na wana sifa za kubadili kada ama kupadishwa daraja wanakwamishwa kwa sababu za mtu binafsi.

“Nisisiitize waajiri, tuwape fursa wafanyakazi wetu, wabadilishe kada, kwani inawapa motisha ya kuongeza ari ya kazi na kujituma ili kuongeza juhudi za maendeleo kwenye mkoa wetu.

“Niwasihi na kuwatia moyo watumishi, wanaotamani kubadilisha kada, wajiendeleze kwenye kada ambayo wanataka Kwenda, na kuwasilisha maombi yao kwenye taasisi zinazohusika” amesema.

Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu imefanikiwa kuwapandisha madaraja watumishi 15,553 tangu ilipoingia madarakani mpaka kufikia Desemba mwaka 2025.

Amesema pia jumla ya wafanyakazi 1,194 wamebadilishiwa kada baada ya kujiendeleza kielimu na wengine kuomba kubadili kada ya utumishi kutokana na kukidhi matakwa ya kitaaluma.

Amesema kwa serikali ya awamu ya sita mkoa wa Geita umepata ajira mpya 4,418 huku watumishi 324 wakipata mafunzo ya muda mfupi na watumishi 525 wakipeta mafunzo ya muda mfupi.

Amesema pia watumishi 1,750 wamelipwa malimbikizo ikiwemo sh bilioni 4.4 ambayo ni malimbikizo ya uhamisho na safari huku sh bilioni 6.4 ikiwa ni malimbikizo ya mishahara.

Akizungumza kwa niaba ya TUCTA, Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Geita, Pauline Tinda ameiomba serikali ifanye malipo ya posho za safari na uhamisho kwa wakati.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I have even managed $20880 merely calendar month by simply working some easy tasks from my apartment. As I had lost my office career, I was very disturbed but luckily I’ve discovered this best on-line career that’s why I’m capable to own thousand USD just from home. Each person can avail this best offer & collect more greenbacks online checking this
    web……w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button