Dk Mecktridis alia na shida ya maji Malinyi

Aishukuru Serikali kwa hatua zilizochukuliwa mpaka sasa

DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Malinyi, Dk. Mecktridis Mdaku, ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za miradi ya maji katika jimbo lake, huku akiibua changamoto kadhaa zinazoendelea kuwakabili wananchi.

Akichangia moja kwa moja bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji, Dk. Mecktridis amesema fedha zilizotolewa zimewezesha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya Malinyi, Misegesi, Ihowanja, Biro, Mchangani, Kilosa Mpepo na Mbalinyi.

Hata hivyo, ameomba Serikali kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya miradi ya maji ya Mserereko wa Mtimbira na Itete, iliyojengwa miaka ya 1980, akieleza kuwa kwa sasa inahudumia zaidi ya watu 72,000 badala ya 12,000 wa awali.

Aidha,ameeleza kuwepo kwa uhaba mkubwa wa maji katika maeneo ya pembezoni ikiwemo Madega, Njasa, Lumbanga, Mkanga, Butu na Shinyanga, na kuomba Serikali kupeleka miradi ya visima ili kuondoa adha kwa wananchi.

Dk. Mecktridis amesisitiza kuwa hatua za haraka zinahitajika ili kuboresha huduma ya maji kwa lengo la kukidhi mahitaji ya wananchi wa Malinyi.

Pia ameitaka Serikali kushughulikia madeni ya wakandarasi ili kuzuia kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya maji.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button