Kilomita 985 barabara ya Nyang’hwale zaidhinishwa

GEITA: SERIKALI imeidhinisha mtandao wa barabara mpya zenye urefu wa Km 985.28 katika Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita zitakazohudumiwa na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA).

Meneja wa TARURA wilayani Nyang’hwale, Mhandisi John Msita ametoa taarifa hiyo wakati wa kikao cha tatu cha Baraza la Madiwani la kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/26.

Mhandisi Msita amesema mtandao huo ni sehemu ya mapendekezo ya barabara mpya zilizohitaji kusajiliwa na kuhakikiwa ili ziingizwe kwenye mtandao wa barabara unaohudumiwa na TARURA.

Amesema katika kuboresha mtandao wa barabara mwaka 2024/25, TARURA wilayani humo ilipokea kiasi cha sh bilioni 1.3 sawa na asilimia 77.9 ya bajeti iliyoidhinishiwa Sh bilioni 1.7.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2025/26 hadi Aprili 2026 tayari wamepokea sh milioni 211 sawa na asilimi 13 kati ya sh bilioni 1.5 ya fedha ya matengenezo ya barabara iliyoidhinishwa.

Akichangia taarifa hiyo, Diwani wa Kata ya Nyamtukuza, Gervas Mabesa ameiomba TARURA kufanya ufuatiliaji kwa wakandarasi wanaopewa kandarasi ujenzi na ukarabati wa barabara.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

  2. Have you ever thought about adding a little bit more than just your articles?
    I mean, what you say is important and everything. However imagine
    if you added some great photos or video clips to give your posts more, “pop”!

    Your content is excellent but with images and clips, this blog could certainly be one of the best in its field.
    Excellent blog!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button