Wanafunzi watakiwa kuwa mstari wa mbele kupinga rushwa

ARUSHA: WAKUU wa shule wametakiwa kuhamasisha wanafunzi kujiunga na klabu za wapinga rushwa ili kuwajengea maadili mema, uzalendo na kuwafanya kuwa mabalozi wa kupinga vitendo vya rushwa katika jamii.
Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Wazo Mwang’onda wakati wa uzinduzi wa klabu za wapingarushwa katika Shule ya Sekondari Migungani One iliyopo Wilaya ni Monduli.

Amesema endapo wanafunzi watashiriki kikamilifu katika klabu hizo watapata elimu ya kupinga rushwa na kuwa chachu ya mabadiliko katika familia, shule na jamii kwa ujumla.

Walimu wakuu wametakiwa kushirikiana na taasisi husika kuhakikisha klabu hizo zinaanzishwa na kuimarishwa katika shule zote ili kujenga kizazi chenye maadili kitakachochangia maendeleo ya taifa.
Aidha, uzinduzi huo ulienda sanjari na kufungua mradi wa umaziliaji wa vyumba vinne vya madarasa kwa ajili ya mapokezi ya kidato cha kwanza cha 2028 ambapo halmashauri hiyo inatarajia kupokea wanafunzi 10,057 huku shule hiyo ikitarajia kupokea wanafunzi 2028.



