Serikali yakemea ufugaji holela wa punda mitaani

GEITA: SERIKALI imekemea tabia ya ufugaji holela wa wanyama aina ya punda usiozingatia huduma, makazi na malazi stahiki kwa wanyama hao hali inayopelekea kuhatarisha afya, usalama na maisha ya punda nchini.
Aidha serikali imeagiza jamii kushiriki kutoa taarifa na kudhibiti shughuli na biashara haramu zinazoongeza athari na hatari ya mnyama punda kutoweka nchini na duniani kwa ujumla.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mkuu wa wilaya ya Geita, Hashimu Komba alitoa kauli hiyo juzi kwa niaba ya serikali katika maadhimisho ya siku ya punda kitaifa yaliyofanyika wilayani Geita.
Maadhimisho hayo yaliratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na INADES Formation Tanzania, Shirika la Ustawi wa Wanyama la Arudha (ASPA) na Ufadhili wa Brooke East Africa.
Komba amesema serikali hairuhusu ufugaji holela unaopelekea punda kuzagaa mitaani bila makazi maalum pamoja na utumikishaji uliopita kiasi unaoathiri afya na ustawi wa maisha ya punda.
“Lazima mnyama punda awe na sehemu sahihi ya kutunzwa, wapo wafugaji ambao wanafuga punda, punda ameshamfanyia kazi asubuhi hadi jioni, amefikisha mizigo, anamtelekeza”, amesema.
Aidha ametaja changamoto nyingine ya ufugaji wa mazoea wa mazoea ni punda kukosa matibabu ya kiafya, kutopewa huduma za chakula na maji mara baada ya utumikishaji uliokithiri.
“Lazima tukubaliane namna bora ya kumtunza mnyama punda, mnyama ambaye ni muhimu sana kwa ustawi wa shughuli mbali mbali za kiuchumi katika maeneo yetu”, amesema.
Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji, Dk Elfas Msenya amesema huduma ya afya na elimu ya wanyama kazi inapaswa kuwa endelevu chini ya usimamizi wa maofisa mifugo kata.
Daktari wa Mifugo kutoka Taasisi ya INADES, Charles Bukula amesema katika kuazimisha siku ya punda duniani, jumla ya punda 200 wamepatiwa tiba huku wananchi 1,000 wakipewa elimu maalum mkoani Geita.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania, Shaaban Tuzzo amesema maazimisho ya punda Tanzania yalianza mwaka 2024, na huazimishwa Mei 05 ya kila mwaka ili kulinda asili ya punda.
Mwenyekiti wa Wanyama Kazi kata ya Mgusu, Emmanuel Charles amesema eneo hilo lina zaidi ya Wanyama kazi zaidi ya 800 ambao wanafanya shughuli mbalimbali kwenye maeneo ya migodini.
Charles amesifu hatua ya ASPA kutoa elimu ya usimamizi na ufugaji sahihi wa Wanyama kazi aina ya punda ambpo imepunguza vifo vya punda baada ya jamii kupata uelewa wa huduma stahiki.




I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
This is what I do….. ………… https://www.work27.info