Elimu usalama barabarani yalenga AFCON 2027

DAR ES SALAAM: MBUNGE wa Jimbo la Mbagala, Burchard Kakulu amesema kampeni ya utoaji elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda itakuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya Tanzania kuelekea mashindano ya 2027 Africa Cup of Nations.

Kakulu amesema hayo katika kampeni ya Usalama Daima iliyofanyika katika viwanja vya Zakhiem Mbagala, Temeke jijini Dar es Salaam, ikiwahusisha waendesha bodaboda maarufu kama maofisa usafirishaji.

“Tunaenda kuandaa mashindano ya Afcon mwakani, kama wenyeji wa mashindano kwa vyovyote vile watu watahitaji kusafiri. Kuna watakaokuwa wanatoka Mbagala kwenda viwanjani kuangalia mpira Benjamin Mkapa, Azam Complex na maeneo mengine.

Semina hii itasaidia watu kusafirishwa kwa usalama zaidi,” amesema Kakulu.

Amesema pamoja na maandalizi ya mashindano hayo, elimu ya usalama barabarani ina umuhimu mkubwa katika kuokoa maisha ya wananchi na kuimarisha maendeleo ya taifa.

“Katika maisha hata ungekuwa na maono mazuri, ndoto kubwa na mawazo mazuri kiasi gani, kama hauko salama kiafya havina maana yoyote. Tunapookoa maisha ya watu tunaokoa maendeleo,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button