Tume yapokea malalamiko 29, yaendelea kuchunguza

SHINYANGA: TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeeleza kupokea malalamiko 29 ya aina mbalimbali kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid ambayo baadhi yake watakwenda kuyafanyia uchunguzi na kuendelea kutoa elimu ya msaada wa kisheria.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa Mfawidhi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kanda ya Ziwa ikiwemo Mkoa wa Shinyanga, Gordian Bunamungu huku akieleza ndani ya wiki moja malalamiko hayo yaliyowafikia na mengine waliweza kuyatatua hapo hapo.

Binamungu amesema malalamiko hayo 29 yalihusiana na migogoro ya ardhi,ndoa utunzaji wa watoto na utumiaji vibaya wa madaraka kutoka kwenye taasisi za umma za serikali na binafsi na kutoa elimu ili kuhakikisha kila mmoja anapata haki.

“Kupitia kauli mbiu ya msaada wa kisheria kwa haki,usawa,amani na maendeleo na sisi tume ya haki za binadamu na utawala bora tunatoa huduma bure tunasisitiza wananchi waendelee kupata elimu ili wajue haki zao za msingi,”amesema Binamungu.

Mkazi wa kata ya Ndembezi Bakaro Lwanda amesema wao wamepeleka malalamiko kwenye tume ya haki za binadamu baada ya kupewa tenda ya ujenzi wa vyumba vya madarada shule za sekondari za Mwambasha na Mwasingu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kumaliza mkataba fedha za ukamilishaji tangu mwaka jana mkurugenzi wa halmashauri hiyo anawazungusha hataki kuwalipa.

Mkazi wa Kata ya Ngokolo, Mwajabu Ally akiwakilisha wenzake amesema mgogoro wa kiwanja umedumu miaka 30 baada ya mtu wanayedai kuchukua eneo lao alieleza kupewa na ofisi ya manispaa kila siku wamekuwa wakizungushwa hawapati muafaka wa kupata haki yao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button