Zaipuna kueleza mageuzi ya NMB Cambridge

DAR ES SALAAM: Katika hatua muhimu kwa sekta ya benki nchini na uongozi wa taasisi za kibiashara barani Afrika, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna anatarajiwa kuzungumza katika Jukwaa la Mkutano wa Biashara Afrika 2026 utakaofanyika Mei 30, 2026 nchini Uingereza.

Katika jukwaa hilo, Zaipuna anatarajiwa kutoa hotuba kuu kuhusu safari ya mageuzi ya NMB na mchango wake katika uchumi wa Tanzania, akieleza namna benki hiyo ilivyokua kutoka katika mizizi ya huduma ndogo za fedha hadi kuwa moja ya taasisi zinazoongoza katika sekta ya fedha nchini.

Mkutano huo wenye kaulimbiu ya “Kujenga Mustakabali wa Afrika: Mitaji, Ubunifu na Ukuaji wa Kiwango cha Bara,” unalenga kujadili nafasi ya Afrika katika kuchochea ukuaji kupitia mitaji, ubunifu na uwezo wa taasisi za Afrika kufanya kazi kwa kiwango cha bara, hususan katika mazingira ya AfCFTA.

Akizungumzia mwaliko huo, Zaipuna amesema ni heshima kwa NMB na Tanzania, akibainisha kuwa safari ya benki hiyo inaonesha kuwa taasisi zinazoongozwa na waafrika zinaweza kujenga ubora wa kiwango cha dunia huku zikibaki karibu na mahitaji ya wananchi, biashara na vipaumbele vya taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button