Watunga sera, watafiti kujadili mafaniko TRA kesho

DAR ES SALAAM: WATUNGA sera, watafiti, wataalamu wa kodi, wawakilishi wa sekta binafsi, walipa kodi na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajia kukutana kesho Dar es Salaam kujadili mafanikio ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Majadiliano hayo yatalenga mafanikio yaliyopatikana katika miaka 30 ya usimamizi wa mapato na kuweka dira ya maendeleo kwa miaka 30 ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 18, Kaimu Mkuu wa  Chuo Cha Kodi Tanzania, Dk Lewis Ishemoi, amesema mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha, Balozi Dk Balozi Khamis Mussa Omar ambaye atazindua mijadala mbalimbali kuhusu maendeleo ya usimamizi wa kodi.

Kwa mujibu wa waandaaji, washiriki watapata fursa ya kujadili mafanikio yaliyopatikana katika miongo mitatu ya mageuzi ya usimamizi wa kodi, mchango wa teknolojia katika kuboresha huduma za kodi, pamoja na mafunzo na uzoefu uliopatikana katika kipindi hicho.

SOMA ZAIDIhttps://habarileo.co.tz/tra-yasisitiza-mazingira-bora-ya-kazi-kuimarisha-ufanisi/

Aidha, kongamano hilo litajadili mikakati ya kupanua wigo wa kodi, kuimarisha ulipaji wa kodi kwa hiari, kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa kodi na kuimarisha ushirikiano kati ya TRA na wadau mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Aidha, amesema kongamano hilo linafanyika wakati TRA ikiadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, hatua inayotoa nafasi ya kutafakari safari ya mamlaka hiyo, mafanikio yake na mwelekeo wake wa baadaye.

SOMA ZAIDIhttps://habarileo.co.tz/tra-yakusanya-tril-9-31-miezi-mitatu/

TRA imewataka washiriki wote walioalikwa kuhudhuria kongamano hilo ili kwa pamoja kujadili mafanikio yaliyopatikana na kuweka misingi imara ya kuimarisha zaidi usimamizi wa mapato na huduma za kodi katika miongo ijayo.

Kongamano hilo linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, mawazo na mapendekezo yatakayochangia kuongeza ufanisi wa mfumo wa kodi na kukuza maendeleo ya uchumi wa taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button